WAZIRI WA MICHEZO ITALIA AMTAKA MKUU WA SPOTI AONDOKE
Waziri wa michezo nchini Italia Andrea Abodi, amemtaka mkuu wa shirikisho la soka nchini humo kujiuzulu baada ya timu ya taifa ya soka ya taifa hilo, the Azzurri, kukosa kushiriki kombe la dunia kwa mara ya tatu mtawalia.
Mabingwa hao wa dunia mara 4, walibanduliwa kupitia mechi ya mwondoano kwa mara nyingine tena baada ya kukosa tiketi ya moja kwa moja kupitia mechi za makundi, mara hii wakiangushwa na Bosnia and Herzegovina Jumanne usiku na kuwaacha wachezaji kwa machozi na mshangao.
Italia hawatakuwa nchini Marekani, Mexico na Canada kwa kombe la dunia mwezi Juni mwaka huu, wakiwa mabingwa wa awali wa dunia wa kwanza sambao wamekosa kushiriki dimba hilo mara tatu mfululizo.
Mkuu wa shirikisho hilo Gabriele Gravina, alisema hatajizulu ila huenda akatimuliwa kwenye mkutano wa bodi wiki ijayo.
Hata hivyo, Abodi amekiri kuwa kandanda ya Italia inapaswa kujengwa upya kuanzia chini kuenda juu, ikianza na mabadiliko ya uongozi katika shirikisho la soka.
Duru zinaarifu kuwa kocha wa timu hiyo Gennaro Gatusso, ameratibiwa kuondoka muda wowote.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































