KSSA: ST ANTONY’S YAIBUKA NA USHINDI KWENYE MAGONGO
Shule ya St Antony’s ya Kitale imeanza vyema mashindano ya kitaifa ya michezo ya shule za upili muhula wa kwanza baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya wenyeji Kisumu Day.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali, nyota wa timu hiyo Kevin Onyango alifunga bao pekee lililoipa ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya wapinzani wao.
Kocha wa timu hiyo Kevin Lugalia amesema wanapania kurejesha ubingwa waliotwaa mwaka 2022 huku wakijiamini kuendelea vyema katika mashindano hayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































