#Local News

KAGWE ATOA HAKIKISHO LA MBEGU

Wizara ya kilimo nchini imewataka wakulima kuondoa hofu kuhusiana mbegu, ikisema kuna akiba ya kutosha za upanzi msimu huu na mwaka mzima.

Waziri wa kilimo Mutahi Kagwe, amesema kuwa serikali imeimarisha mikakati ya uzalishaji na usambazaji wa mbegu katika juhudi za kuhakikisha kila mkulima anafikiwa na mbegu kwa wakati.

Amesema uwekezaji zaidi unaendelea katika sekta ya kilimo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *