KENYA YAZINDUA MPANGO WA KUIMARISHA USIMAMIZI WA TABIANCHI WA KAMPUNI
Serikali kuu imezindua mpango wa “Chapter Zero” unaolenga kuimarisha usimamizi wa tabianchi katika sekta ya kampuni mbali mbali.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi Festus Ng’eno akizungumza katika uzinduzi huo mjini Nairobi, amesema kuwa mpango huo unaendeleza hatua za tabianchi na uendelevu wa mazingira.
Ng’eno ameongeza kuwa serikali inakamilisha kanuni za ziada kuhusu masoko ya kaboni, urejeshaji wa ardhi oevu na usimamizi wa taka za kielektroniki ili kuboresha usimamizi wa mazingira na kutoa uwazi kwa wawekezaji.
Aidha amesema juhudi za kitaifa, ukiwemo upandaji wa miti bilioni 15 utasaidia kurejesha mandhari yaliyoharibika, kuboresha hali ya anga na kusaidia maisha.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































