FLICK AFADHAIKA NA UAMUZI WA VAR
Kocha wa Barcelona, Hansi Flick, alionekana kukasirishwa baada ya maamuzi ya kushindwa kuangalia tukio la kushangaza la kugusa mpira kwa mkono katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid, uliomalizika kwa Barcelona kupoteza 2-0.
Defenda wa Atletico, Marc Pubill, aligusa mpira uliopitishwa kwake na kipa Juan Musso kwa mkono wake ili kuutumia kwa ajili ya kuanza tena kwa goli, jambo ambalo Flick alisema lingetakiwa kupewa kadi nyekundu na penati.
Hata hivyo, VAR iliingilia kati kwenye tukio lingine lililohusisha defenda wa Barcelona Pau Cubarsi, aliyepewa kadi ya njano kisha kadi nyekundu baada ya kumkomoa Giuliano Simeone, na kuiacha Barcelona wakiwa na wachezaji 10 kipindi cha pili.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































