#Local News

KINDIKI AMULIKWA KUHUSU HELIKOPTA ZA MILIONI 8

Wabunge wameibua maswali kuhusu matumizi ya shilingi milioni 8 zinazogharamia safari za helikopta za kila siku za naibu Rais Kithure Kindiki kwenye kaunti za Isiolo, Laikipia, Kitui na Tharaka Nithi.

Wakati wa vikao vya kuchunguza madeni ya shilingi milioni 478 inayodaiwa afisi ya naibu Rais, wanachama wa kamati ya uhasibu bungeni wametilia shaka faida zinazotokana na matumizi ya fedha hizo, wakitaja kuwa ubadhirifu.

Hata hivyo, baadhi ya wanakamati hiyo wametetea safari hizo hasa katika kaunti ya Tharaka Nithi anakotoka Kindiki.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *