#Local News

POLISI WACHUNGUZA KIFO CHA MTOTO MTAANI BURUBURU

Polisi katika jiji la Nairobi wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha mtoto wa miaka tisa kilichotokea katika eneo la Buruburu chini ya mazingira yasiyoeleweka.

Kwa mujibu wa polisi, mtoto huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa Gredi ya kwanza katika Shule ya Msingi ya Kaloleni alitoka nyumbani tarehe kumi Aprili majira ya saa nne asubuhi kwenda kucheza kabla ya kurejea jioni akiwa na majeraha kichwani na mkononi.

Mama yake alimpeleka katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki Hospital baada ya kulalamikia maumivu ya tumbo, ambapo alifariki alipowasili, huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha majeraha hayo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *