LIVERPOOL YAKABILIWA NA KIBARUA KIGUMU ULAYA
Liverpool wanakabiliwa na kibarua kigumu kuondoa mabingwa watetezi Paris Saint-Germain katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya, lakini wanatumai uwanja wao wa nyumbani utawapa matumaini mapya.
Timu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi ya Uingereeza na imeshindwa kufanya vyema katika mashindano ya ndani, hivyo mashindano ya Ulaya yamebaki kuwa nafasi yao ya mwisho ya kutwaa taji.
Hata hivyo, Liverpool wapo nyuma baada ya kufungwa mabao mawili kwa bila katika mkondo wa kwanza uliochezwa Paris, lakini wanaamini wanaweza kubadili matokeo hayo nyumbani kama walivyowahi kufanya hapo awali.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































