UN YAZINDUA MRADI WA KUBORESHA MAGEUZI YA KIJANI NCHINI KENYA
Shirika la mazingira la umoja wa mataifa (UNEP) na shirika la makazi la umoja wa mataifa (UN-habitat) yamezindua mradi wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 5.2 kubadili mji mkuu wa kenya, nairobi, kuwa kituo cha unyumbukaji wa mabadiliko ya tabianchi, ukuaji chanya wa asili na mfumo wa mzunguko.
Ukifadhiliwa na kituo cha mazingira duniani, mradi huo wa miaka mitano utaongoza mtazamo ya maingiliano ya maeneo ya kijani katika eneo la kamukunji, kwa lengo la kuboresha mazingira ya maisha kwa zaidi ya wakazi 85,000.
Mradi huo utatekelezwa kwa pamoja na unep, un-habitat na mamlaka za serikali ya kenya. wakati wa utekelezaji wake, mradi huo utatoa suluhisho halisi kama miundombinu nyumbufu kwa hali ya hewa, maeneo ya wazi ya kijani, mzunguko wa mfumo wa ikolojia, nishati safi, na usimamizi wa taka.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































