EACC YAJITETEA DHIDI YA UFISADI
Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imetetea utendakazi wake ikisema imepata mafanikio katika hukumu za kesi na urejeshaji wa fedha za umma zilizoibwa.
Mkurugenzi Mkuu Abdi A. Mohamud amesema tume hiyo imefanikiwa kupata asilimia 72 ya hukumu za hatia katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kurejesha shilingi bilioni saba nukta nane za fedha za umma.
Hata hivyo, ameonya kuwa ufisadi bado unaongezeka, akibainisha kuwa zaidi ya shilingi bilioni kumi nukta saba zimepotea katika kipindi hicho, hali inayodhihirisha changamoto zilizopo katika vita dhidi ya ufisadi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































