#Local News

SERIKALI YATAKIWA KUPUNGUZA BEI YA MAFUTA

Serikali imeshinikizwa kuweka mikakati mwafaka ili kuwalinda wakenya dhidi ya gharama ya juu ya maisha kwa kuhakikisha kuwa inapunguza bei ya mafuta licha ya shinikizo katika soko la kimataifa.

Katika kikao na wanahabari, mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro ambaye amekuwa mkosoaji wa serikali kuhusu mzigo wa ushuru, ameitaka serikali kuweka ruzuku mbali na kupunguza ushuru wa ongezeko la thamani, VAT.

Wito huo unajiri huku EPRA ikipunguza VAT kwa bidhaa za petroli kutoka asilimia 16 hadi asilimia 13.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *