#Athletics #Sports

AK YATEUA TIMU 2 KUWAKILISHA KENYA MWEZI MEI

Shirikisho la Athletics Kenya limeziteua timu 2 zitakazoliwakilisha taifa katika mashindano mawili makuu ya kuwania ubingwa mwezi ujao baada ya kukamilisha majaribio katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex jijini Nairobi.

Miongoni mwa wanariadha waliochaguliwa ni wa mbio za masafa mafupi, watakaoshiriki mashindano ya ubingwa wa mbio za kupokezana vijiti jijini Gaborone, Botswana.

Timu nyingine ni wanariadha watakaoiwakilisha Kenya katika mashindano ya kuwania ubingwa wa mbio barani Afrika, wanariadha chipukizi wakiteuliwa kupewa nafasi ya kujitangaza kwa ulimwengu.

Mashindano ya World Relays yanaandaliwa barani Afrika kwa mara ya kwanza, wenyeji Botswana, Kenya, Nigeria na Afrika Kusini wakitarajiwa kutia fora katika mashindano hayo ya mwezi ujao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

AK YATEUA TIMU 2 KUWAKILISHA KENYA MWEZI MEI

OBURU ATOA KAULI KUHUSU MAFUTA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *