KITUYI AANGAZIA NGUVU YA KUNDI LA LINDA MWANANCHI
Msemaji wa muungano wa upinzani Mukhisa Kituyi amesema ushawishi unaoongezeka wa kundi la Linda Mwananchi ndani ya chama cha ODM hauwezi kupuuzwa huku juhudi zikiendelea za kuunda muungano imara kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka elfu mbili ishirini na saba
Kituyi amesisitiza umuhimu wa kuzingatia kundi hilo linaloongozwa na Edwin Sifuna akibainisha kuwa umaarufu wake unaoongezeka umelifanya kuwa sehemu muhimu katika mwelekeo wa siasa za upinzani
Aidha amesema kuwa kihistoria vyama vya upinzani nchini huungana karibu na kipindi cha uchaguzi akieleza kuwa mgawanyiko unaoshuhudiwa kwa sasa si jambo la ajabu katika siasa za Kenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































