RUTO AELEZA KIINI CHA KIWANDA CHA MAFUTA TANGA
Rais William Ruto ametetea pendekezo la kuanzishwa kwa kiwanda cha kikanda cha kusafisha mafuta mjini Tanga nchini Tanzania, akisema pendekezo hilo halikuwa uamuzi wa upande mmoja bali ni sehemu ya majadiliano mapana kuhusu viwanda na matumizi ya raslimali za kikanda.
Akizungumza wakati wa mazungumzo ya pamoja na mwenzake wa Tanzania Samia Hassan jijini Dar es Salaam, Ruto amesema ukaribu wa mji wa Tanga na Mombasa wa takribani kilomita 190, unafanikisha matumizi ya vifaa vinavyoweza kusaidia katika ujumuisha wa miundombinu ya mafuta.
Haya yalijiri baada ya Samia kudai kuwa hakushauriwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































