#Athletics #Sports

MUNGUTI ALENGA KUTIFUA KIVUMBI SHANGHAI

Bingwa wa kitaifa wa mbio za mita 1,500 mwaka wa 2023 Daniel Munguti, ana matumaini ya kuanza safari yake ya kuwinda ubingwa kimataifa kwa kishindo, atakaposhiriki mbio za mita 3,000 katika mashindano ya Diamond League ya Shanghai baadaye mwezi huu.

Munguti alianza kampeni ya msimu wake kwa kumaliza wa tatu katika mbio za Kip Keino Classic mwishoni mwa mwezi jana, nyuma ya bingwa wa dunia na Olimpiki katiki katika mbio za mita 800 Emmanuel Wanyonyi, na mshindi wa nishani ya shaba katika mbio za mita 1,500 ulimwenguni Reynold Cheruiyot.

Kabla yah apo, Munguti alikuwa sehemu ya kikosi cha wenzake Cheruiyot, Winfred Mbithe na Purity Chepkirui kilichomaliza katika nafasi ya 4 katika mbio za kupokezana vijiti kwenye mashindano ya World Cross Country Championship jijini Tallahassee nhcini Marekani mapema mwaka huu.  

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 31, amefichua kwamba mbio za Shanghai zitakazoandaliwa tarehe 16 mwezi huu, zitaashiria mwanzo wa kampeni yake katika ramani ya ulimwengu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *