#Local News

KNCCI NA COTU WAPINGA BAADHI YA MAPENDEKEZO YA MSWADA WA FEDHA

Chama cha Kitaifa cha Biashara na Viwanda Kenya kimeonya kuwa sera ya ushuru iliyopendekezwa katika Mswada wa Fedha 2026 inaweza kudhoofisha ushindani wa uchumi wa Kenya.

Chama hicho kimesema ushuru mpya unaweza kuongeza gharama za biashara na kuathiri uwezo wa kampuni kushindana katika soko la ndani na la kimataifa.

Kwa upande wake, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (COTU) kimesema mswada huo unaipa Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru Kenya mamlaka makubwa mno dhidi ya walipa ushuru hasa katika masuala ya marejesho ya kodi na rufaa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *