MWANAUME MACHKOS ATAKA HAKI BAADA YA KUCHOMWA NDEVU
Mwanaume mmoja mjini Machakos anayefahamika kama John Kyalo anataka haki baada ya kuvamiwa na kuchomwa ndevu alipokuwa amepumzika katika eneo moja mjini humo.
Kyalo amesema mtu anayedai kumfahamu aliwasha moto kwenye ndevu zake ambazo amekuwa akizitunza kwa miaka mingi.
Tukio hilo sasa limezua mjadala huku akiitaka sheria kuchukua mkondo wake dhidi ya mhusika.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































