TUZO YA BALLON D’OR KUFANYIKA LONDON
Sherehe za utoaji wa tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2026 zitafanyika kwa mara ya kwanza jijini London Oktoba 26 kuadhimisha miaka 70 tangu tuzo hiyo ilipotolewa kwa mara ya kwanza mwaka 1956.
Waandalizi wamesema hafla hiyo itaadhimisha kumbukumbu ya mwanasoka wa Uingereza Stanley Matthews aliyekuwa mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo.
Katika miaka ya hivi karibuni, tuzo hiyo imekuwa ikitawaliwa na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo huku mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Ousmane Dembele akitwaa tuzo hiyo mwaka uliopita.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































