BODA BODA WAFUNGA BARABARA MLOLONGO
Shughuli za usafiri zimetatizika kwa muda kufuatia maandamano ya wahudumu wa boda boda katika eneo la Mlolongo kwenye barabara kuu ya Nairobi kuelekea Mombasa wakilalamikia kuteketezwa kwa pikipiki za wenzao kwenye maandamano ya jana.
Kulingana na ripoti za polisi, pikipiki 5 ziliteketezwa wakati wa maandamano ya jana, tukio ambalo limesababisha machungu miongoni mwa wahudumu hao.
Maandamano hayo yamesababisha watumiaji wa barabara hiyo kutumia barabara ya Nairobi Expressway.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































