KENYA POWER YATANGAZA GIZA
Kampuni ya kusambaza umeme Kenya Power imeonya kuhusu ukosefu wa nguvu za umeme katika maeneo kadhaa nchini hii leo kutokana na ukarabati wa mitambo kuanzia saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya maeneo ambayo yataathirika na kukatizwa kwa umeme ni Pamoja na Nairobi, Bomet, Nandi, Kakamega, Homa Bay, Embu, Kirinyaga, na Murang’a.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu ya mtaa wa South C itaathirika kati ya saa tatu huiku maeneo ya Kapset na Kimulot katika kaunti ya Bomet vile vile takiathirika na ukarabati huo.
Sehemu za eneo la Mlango katika kaunti ya Nandi zitakosa umeme kati ya saa nne asubuhi na saa kumi alasiri.
Sehemu za eneo la Musanda katika kaunti ya Kakamega zitaathirika kati ya saa tatu na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Ndhiru, Opinde na Obuya katika kaunti ya Homa Bay yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Kivwe, Kevote na Ndatu katika kaunti ya Embu yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.
Katika kaunti ya Kirinyaga, maeneo ya Karira, Ndorome na Marura yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Makuyu, Kirimiri na Ndithini katika kaunti ya Murang’a pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































