FANYA KAMA COVID, WIZARA YA AFYA
Wizara ya afya imezitaka serikali za kaunti kuweka mikakati ya kuwatenga wagonjwa wa Mpox jinsi ilivyokuwa kwa wagonjwa wa vurusi vya Covid 19.
Katika kikao na wanahabari, katibu mkuu katika wizara ya afya Mary Muthoni, amesema serikali kuu itashirikiana na serikali hizo kukabili maambukizi ya ugonjwa huo.
Tayari shirika la afya ulimwenguni WHO na shirika la kukabili maambukizi ya mgaonjwa barani Afrika CDC, yametangaza Mox kuwa dharura.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































