SHEREHE ZA MADARAKA
Rais william ruto amewasili katika uwanja wa Wajir kwa ajili ya sherehe za siku ya madaraka ya 2026, ikiwa ni mara ya kwanza kwa hafla ya kitaifa kufanyika katika eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya.
Maadhimisho ya siku ya madaraka ya mwaka huu yatafanyika chini ya kaulimbiu, “elimu, ujuzi na mustakabali,” huku serikali ikisema tukio hilo linalenga katika kujifunza, uvumbuzi na ukuzaji wa ujuzi.
Wajir inaandaa sherehe za siku ya madaraka kwa mara ya kwanza katika historia, hatua ambayo serikali inasema inaonyesha kujitolea kwake kwa maendeleo jumuishi na ujumuishaji wa kitaifa.
Serikali pia imefanya maboresho makubwa katika mji wa Wajir, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, taa za barabarani, miunganisho ya maji na ukarabati katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Wajir katika maandalizi ya tukio la kitaifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































