KIRITIMATI YAKARIBISHA 2026!

Kisiwa cha Kiritimati yaani Christmas islands kimekuwa sehemu ya kwanza ya ulimwengu kuukaribisha mwaka mpya wa 2026. Kisiwa hicho kilichoko katika taifa la Kiribati katika bahari ya Pacific kusini mwa Hawaii na kaskazini mashariki mwa taifa la Australia, kilipata uhuru wake kutoka taifa la Uingereza mwaka 1979, na kina takribani wakazi 116. New Zealand imekuwa […]

WAKILI MAHAKAMANI KUZIMA MUZIKI WA “NGANYA”

Wakili mmoja jijini Nairobi kwa jina Samuel Barongo amewasilisha kesi katika mahakama kuu akitaka amri itolewe kuzuia magari ya uchukuzi wa umma kucheza muziki kwa sauti ya juu, akihoji kuwa mwenendo huo unakiuka vipengee kadhaa vya katiba. Kwenye ombi lake, wakili huyo ameukosoa muungano wa wamiliki wa matatu, mamlaka ya usalama barabarani NTSA, ile ya […]

SHINYALU YAENDELEA KUOMBOLEZA

Wakazi katika eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega wataukaribisha mwaka mpya wa 2026 huku wakiomboleza kifo cha aliyekuwa mbunge wao Daniel Khamasi, ambaye wamemtaja kama kiongozi aliyeleta mageuzi eneo hilo. Wakiongozwa na kaka yake James Khamasi, wakazi hao wamemkumbuka mwendazake aliyehudumu kati ya mwaka wa 1997-2007 kutokana na mchango wake katika sekta ya elimu. […]

TANZANIA WAINGIA HATUA YA MWONDOANO

Timu ya Taifa Stars ya Tanzania ilivua vazi la timu ndogo katika mashindano yanayoendelea ya taifa bingwa barani Afrika AFCON 2025 baada ya kutoka nyuma na kulazimisha sare ya bao 1 dhidi ya miamba Tunisia, na kutinga awamu ya mwondoano ya mashindano hayo jana usiku. Hiyo ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kufika awamu […]

ARSENAL YATIA BREKI REKODI YA VILLA

Klabu ya Arsenal ilitamatisha rekodi ya ushindi wa mechi 11 mfululizo wa Aston Villa kwa kuicharaza mabao 4-1 katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza EPL jana usiku huku Chelsea na Manchester United wakipoteza fursa ya kuingia top 4. Mechi hiyo ilikuwa ya Arsenal kulipiza kichapo cha pekee katika mechi 25 kwenye mashindano yote ilichopokezwa […]

American Roulette Online USA from Real Casino

American roulette is one of the most popular casino games in the United States, both in brick-and-mortar casinos and online. With its exciting gameplay and the potential for big wins, it’s no wonder players keep coming back for more. In this article, we’ll take a closer look at American roulette online USA from real casinos, […]

MUSYOKA: MWANIAJI WA UPINZANI KUTAJWA MAPEMA 2026

Mwaka mpya wa 2026 unatarajiwa huku mawimbi ya kisiasa yakitarajiwa kubadilika, muungano wa upinzani ukiahidi kuweka wazi mwaniaji wake wa urais katika kipindi cha miezi 3 ya kwanza ya mwaka huo. Katika taarifa yake ya mwisho wa mwaka kwa taifa, kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka ametoa hakikisho kuwa muungano huo utasalia Pamoja, huku akionyesha matumaini […]

WAKENYA HAWANA LA KUJIVUNIA 2025- UTAFITI

Wengi wa Wakenya ambao ni zaidi ya asilimia 80 hawana lolote walolofurahia mwaka huu unaotamatika kwa 2025, wakirejelea masaibu waliyosababishiwa na gharama ya juu ya maisha kama chanzo kikuu kilichowanyima furaha. Kwa mujibu wa utafiti wa shirika la Infotrak uliofanywa mwezi huu, Wakenya aidha wamelalamikia ufisadi, sera za serikali na ushuru wa juu wanaotozwa pia […]

WAZAZI: WATOTO WETU WAMESHUSHWA HADHI

Wazazi wa wanafunzi wanaojiunga na sekondari ya juu wameendelea kulalamikia dosari katika shule walizowekwa wanao, huku zikiwa zimesalia wiki 2 pekee kabla ya wanafunzi hao kuripoti kwenye shule walizowekwa. Miongoni mwa malalamishi ni wanafunzi kuwekwa kwenye shule za hadhi ya chini ikilinganishwa na matokeo yao ya tathmini ya KJSEA, wakitaka wizara ya elimu kufanya marekebisho. […]

VIONGOZI WASHINIKIZA ‘AJALI’ YA JIRONGO ICHUNGUZWE

Baadhi ya viongozi kutoka Magharibi mwa nchi wameendelea kutilia shaka kifo cha aliyekuwa mbunge wa Lugari Cyrus Jirongo kwenye ajali ya barabarani, licha yake kuzikwa hapo jana. Wakizungumza kwenye hafla ya mazishi, viongozi hao akiwemo seneta wa Kakamega Boni Khalwale na mwenzake wa zamani wa Vihiga George Khaniri, wameitaka idara ya usalama kufanya uchunguzi huru […]