MHUDUMU WA MPESA APIGWA RISASI KATIKA TUKIO LA UHALIFU MUKURWEINI NYERI

Polisi wanaendelea kuwasaka watu waliompiga risasi Mhudumu wa Mpesa na kujeruhiwa katika tukio la wizi katika Mji wa Kiahungu, Kaunti ya Nyeri. Kulingana na polisi, mwanamke huyo alikuwa akirejea nyumbani baada ya shughuli za siku, akiwa na mwenzake, walipovamiwa na wanaume wawili, mmoja akiwa na bastola. Wahalifu walimnyang’anya KSh.160,000 taslimu, simu tatu, na bidhaa mbalimbali […]

WAZAZI WASHAURIWA KUTHIBITI MATUMIZI YA MITANDAO KWA VIJANA

Wito umetolewa kwa wazazi kuwashauri wanao kuhusi mathara yanayoweza kutokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii. Kiranja wa wachache katika bunge la kitaifa Milly Odhiambo amewakosoa vijana kufuatia matumizi mabaya ya kijamii kwa kuwashambulia viongozi mitandaoni. Vile vile amekashifu matukio ya hivi majuzi ambapo wakenya wanaokosoa serikali mitandaoni wamekuwa wakitekwa nyara kiholela bila hatua […]

MARY MUTHONI; HAKUNA HMPV KENYA

Wakenya wamehakikishiwa kuwa wizara ya afya inafanya kila iwezalo kuthibiti maambukizi ya ugonjwa wa m-pox. Wizara ya afya aidha imesema kuwa imeimarisha uchunguzi wa HMPV na mpox katika mipaka yote ya kenya. Kwa mujib u wa katibu wa afya ya umma Mary Muthoni serikali imeimarisha uchunguzi wa watu wote wanaokuja humu nchini na kwamba kenya […]

MAN UNITED WAICHARAZA ASENALI 5-3

Wachezaji kumi wa Manchester United waliwalaza Arsenal 5-3 kwa penalti baada ya sare ya 1-1 katika raundi ya tatu ya Kombe la FA. United walilipiza kisasi kufuatia kichapo cha 2-0 kutoka kwa Arsenal kwenye Ligi Kuu mwezi Desemba. Bruno Fernandes aliwaweka United kifua mbele kwa shuti kali dakika ya 52, lakini Diogo Dalot alitolewa nje […]

NAIVAS WAILAZA MSA 4-1 NYUMBANI

Robert Karisa alifunga mabao mawili huku Naivas FC wakiwafunga Mombasa Stars 4-1 kwenye mechi ya Ligi ya Kitaifa ya Daraja la Kwanza (NSL) iliyochezwa Serani, Mombasa. Newton Ochieng na Markvivan Kesa waliongeza mabao mengine kwa Naivas, huku Gabriel Michael akifungia Stars bao la kufutia machozi. Ochieng alifunga bao la kwanza dakika ya 45 kwa shuti […]