WALIMU WA JSS WADAI KUPEWA KANDARASI YA KUDUMU NA TSC

Walimu wa sekondari ya msingi JSS wamefanya maandamano katika kaunti mbali mbali humu nchini kushinikiza serikali kuwaajiri kwa kandarasi ya kudumu. Kulingana na walimu hao tume ya huduma za walimu TSC imekiuka agizo la mahakama kuitaka kuwapa kandarasi ya kudumu baada ya kuhudumu kama walimu wanagenzi kwa Zaidi ya mwaka mmoja unusuMaandamano hayo yanajiri wakati […]

SERIKALI IMEWEKEZA PAKUBWA KATIKA KILIMO ILI KUTATUA UHABA WA CHAKULA NCHINI

Mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa Ndindi Nyoro amesema serikali imewekeza pakubwa katika sekta ya kilimo ili kufanikisha mpango wa utoshelezi wa chakula nchini. Kwa mujibu wa Nyoro bunge linabuni sheria ya kudhibiti bidhaa zinazoagizwa nchini wakulima wakiwezeshwa kuzalisha baadhi ya bidhaa nchini ili kupunguza gharama ya uagizaji. Aidha nyoro ambaye pia […]

NYORO APIGIWA DEBE KUWA NAIBU RAIS 2027

Viongozi mbali mbali wameendelea kumshinikiza mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro kuwa mgombea mwenza wa rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2027. Wa hivi punde ni mbunge wa jumujia ya afrika mashariki EALA David Olesankok akisema Nyoro ana mwonekano wa kitaifa na pia atawakilisha vijana katika ngazi za juu.

NANI ALIYEMUUA MBUNGE WA ZAMANI WA KABETE GEORGE MUCHAI?

Vikao vya kusikiliza kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa mbunge wa Kabete George Muchai vinarejelewa leo hiiWashukiwa sita walioshitakiwa kufuatia mauaji hayo, Eric Isabwa, Raphael Kimani, Mustapha Kimani , Jane Wanjiru, ,washukiwa hao walifunguliwa mashtaka mwaka wa 2015 kesi hiyo ilipoanza rasmi,Sita hao hata hivyo walikana mashtaka dhidi yao na kesema kwamba hawakuhusika katika mauaji […]

DEREVA NA MAKANGA WAKE WATAFUTWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA UMILIKI WA MISOKOTO 60 YA BANGI

Maafisa wa polisi wameanzisha msako wa kuwatafuta na kuwakamatga dereva mmoja na makanga wake kufuatia madai ya misokoto 60 ya bangi yenye dhamani ya shilingi milioni 3 waliyoishusha kutoka kwa lori walilokujwa nayo kando ya barabara eneo la ngorika kauti ya Nyandarua. Inaarifiwa kuwa wawili hao walikuwa wakitorokea polisi kabla ya kushusha shehena hiyo na […]

TUREJESHE WANAFUNZI SHULENI RAIS RUTO AMESEMA

Rais William Ruto ametoa wito kwa wazazi kuwarejesha wanao shuleni akiwahakikishia kuwa mvua kubwa iliyosababisha uharibifu mkubwa na kupelekea kufungwa kwa shule kwa takribani wiki mbili imepungua. Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa shule ya msingi ya Lenana jijini Nairobi Ruto amesisitiza kuwa serikali itaimarisha usalama wawanafunzi,walimu na wafanyakazi shuleni. Ameongeza kuwa serikali kwa ushirikiano […]

GACHAGUA AFUFUA UPYA MDAHALO WA MGAO WA FEDHA WA ONE MAN ONE VOTE ONE SHILLING

Naibu wa rais Rigathi Gachagua amefufua upya mdahalo kuhusu mgao wa fedha za kitaifa akisema maeneo yenye watu wengi yanastahili kupata mgao zaidi kwa mujibu wa mfumo 1man 1 vote 1 shilling. Kwa mujibu wa gachagua baadhi ya maeneo bunge hasa mlima kenya yana idadi kubwa ya watu ilhali yanatengewa mgao mdogo Zaidi.

SHULE KUFUNGULIWA LEO JUMATATU BAADA YA KUAHIRISHWA KWA MUDA

Shule zikifunguliwa leo hii kwa muhula wa pili serikali imetangaza kanuni za usalama kuwalinda wanafunzi, walimu na wafanyakazi wote shuleni. Katika taarifa wizara ya usalama na maswala ya ndani ya nchi imesema shule zilizoadhiriwa Zaidi na mafuriko hazitafunguliwa leo hii hadi serikali itakapozikarabati shule hizo. Raymond omolo ni katibu katika wizara wizara ya usalama na […]

WIZARA YA MAZINGIRA IMETOA RATIBA YA KUENDESHA SHUGHULI YA UPANZI WA MICHE

Wizara ya mazingira imetoa ratiba kuhusu jinsi mawaziri watakavyoongoza shughuli ya upanzi wa miche kuanzia leo jumatatu. Kwa mujimu wa wizara hiyo mwanasheria mkuu wa serikali Justin Muturi ataongoza shughuli ya upanzi wa miche katika msitu wa ngong kaunti ya Kajiado , naye waziri wa elimu Ezekieli Machogu ataongoza shughuli hiyo kesho jumanne katika kaunti […]