KUPPET KWALE;HATUENDI SHULE

Wanachama wa muungano wa walimu wa sekondari na vyuo vya kadri KUPPET tawi la Kwale wamesema kujwa hawatarejea kazini hadi malalamishi yao yatekelezwe yote. Wakiongozwa na Leonard Oranje ambaye ni katibu wa muungano huo tawi la Kwale wameapa kususia kazi hadi matakwa yao yatekelezwe. Imetayarishwa na Janice Marete

STENCY NEEMA AWEKA HISTORIA KWA KENYA KATIKA OLIMPIKI YA WALEMAVU

Mchezaji wa taekwondo wa timu ya taifa ya Kenya, Stency Neema ameshindwa katika Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Paris kufuatia kulemewa 12-3 na mshindi wa medali ya fedha ya dunia ya 2023. Salma Ali Abdi Al Moneem Hassan wa Misri katika hatua ya 16 bora kwa wachezaji walio chini ya kilo 52 kwa wanawake […]

STEPH CURRY AONGEZA MKATABA NA GOLDEN STATE WORRIORS

Mchezaji Nyota wa timu ya Golden State Warriors Stephen Curry amekubali kuongezewa mwaka mmoja kwenye mkataba wake kwa mshahara wa $62.6 milioni (Ksh 8 billion) ili aendelee kusalia na Golden State hadi msimu wa 2026-27. ESPN iliripoti kwamba wakala wa Curry, Jeff Austin, alikuwa amethibitisha dili hiyo kwa mchezaji huyo bora mara mbili wa NBA. […]

LIVERPOOL KUMENYANA NA REAL-MADRID

Liverpool itamenyana na watetetezi wa ligi ya mabingwa real-madrid katika kurejea kwao kwenye kinyanganyiro hicho kufuatia draw ya muonekano mpya. Timu ya manchesta city na arselani zinacheza zote na tim u iliyofuzu katika nusu fainali msimu uliopita katika mechi zao huku aston vila wakichuana na mabingwa Scotland Celtic ,huku kila timu ikicheza mech inane katika […]

KAMATI YA UTENDAJI YA AFC LEOPARDS YABUNI JOPO KAZI LA WATU WANNE

Mwenyekiti wa AFC Leopards Dan Shikanda amefichua kuwa Kamati ya Utendaji ya kitaifa ya klabu hiyo imebuni jopo kazi la watu wanane kubaini iwapo klabu hiyo inapaswa kubadilika kutoka katika mfumo wa kijamii hadi muundo wa ushirika. Shikanda alisema kwamba kikosi kazi hicho kitaanza ziara ya kina ya matawi 85 ya klabu hiyo. Shikanda pia […]

HONGERA POLISI BULLETS KWA KUFIKA FAINALI; KOCHA ODEMBA

Kocha mkuu wa Kenya Police Bullets fc, Beldine Odemba amesifu wachezaji wake kwa kufika fainali ya kuwania kufuzu kwa ligi klabu bingwa afrika ya Wanawake ya Cecafa lakini anasema inauma kwamba walikosa tiketi hiyo. Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake nchini walifungwa 1-0 na CBE ya Ethiopia katika fainali jana mjini Addis Ababa, […]

MAISHA NAMBA SI LAZIMA, BITOK

Wakenya hawawatalazimishwa kujisajili kwenye mpango wenye utata wa maisha namba, huku katibu mkuu katika idara ya uhamiaji Julius Bitok akisema serikali inalenga kutumia mfumo utakaowawezesha wakenya kujisajili kwa kujitolea. Kauli yake imejiri wakati ambapo serikali imekuwa na mpango wa kufutilia mbali vitambulisho vinavyotolewa kwa sasa na kutoa vitambulisho vya Maisha namba kwa wanaotuma maombi. Mbali […]

TULISHAURIANA NA ODINGA KUUNGANISHA NCHI, RUTO

Rais William Ruto amekariri haja ya taifa kuungana na kufanya kazi kwa ushirikiano bila kujali mirengo ya kisiasa, akisema hatua hiyo itasaidia katika kuimarisha utendakazi wa serikali kwa faida ya mwananchi. Akizungumza kwenye kaunti ya Homa Bay wakati wa ziara yake ya maendeleo, Ruto amesema hatua ya kuwajumuisha viongozi wa upinzani kwenye baraza lake iliafikiwa […]

LENOLKULAL ROHO MKONONI HUKUMU IKINUKIA

Gavana wa zamana wa Samburu Moses Lenolkalal anatarajiwa kufahamu hukumu yake muda wowote kuanzia sasa baada ya mahakama inayosikiliza kesi za ufisadi hapo jana kumpata na hatia ya ufisadi unaohusisha shilingi milioni 84. Lenolkulal ambaye alishtakiwa na wenzake 10 ambao pia wamepatikana na hatia, ameiomba mahakama kumpa kifungo cha nyumbani au faini na wala si […]

KAMATI 7 YABUNIWA KUTENGEZA SRC

Rais William Ruto amebuni kamati yenye wanachama 8 watakaohusika katika kuwasajili makamishna wa tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi wa umma SRC, baada ya muhula wa miaka 6 wa makamishna waliokuwepo kutamatika. Wanakamati hao Joshua Wambua, Patrick Mtange, Monica Sifuna, Quresha Abdullahi, Amos Gathecha, Mary Kimonye, Lawrence Kibet na Samuel Kaumba. Mwenyekiti wa sasa Lynn Mengich […]