MSIMAMIZI WA BAJETI APINGA OMBI LA SENETA

Msimamizi wa bajeti ya serikali Margaret Nyakang’o amepinga pendekezo la seneta wa Meru Kathuri Murungi la kutaka amzuie gavana Kawira Mwangaza kutoa fedha za kaunti hiyo kwa akaunti zinazomilikiwa na kaunti hiyo, akisema kwamba Mwangaza angali mamlakani. Kupitia barua iliyoandikwa hapo jana, Nyakang’o amemkumbusha seneta huyo kwamba Mwangaza ana agizo la mahakama linalozuia kutimuliwa kwake […]

WAKAZI KITALE WAHANGAIKA, WAKOSOA KeNHA

Wakazi wa Matisi kaunti ya Tans Nzoia waliotoa ardhi yao kuruhusu ujenzi wa barabara ya Kitale kuelekea Suam mpakani mwa Kenya na Uganda miaka miwili iliyopita, wamelalamikia fidia walioahidiwa na serikali. Wakazi hao ambao maduka yao yalibomolewa kupisha ujenzi huo, wameitaka mamlaka ya barabara kuu nchini KeNHA kufanikisha malipo yao kulingana na mkataba wao na […]

KUPPET YASAMBARATISHA MASOMO BUNGOMA

Viongozi wa chama cha KUPPET kaunti ya Bungoma wamesambaratisha shughulli za masomo katika shule mbalimbali ikiwemo ile ya kitaifa ya wasichana ya Lugulu kwenye kaunti hiyo baada ya kuwafurusha walimu waliokuwa wakiendeleza shughuli za masomo. Wakiongozwa na katibu wa chama hicho kaunti ya Bungoma Augustine Luketero, wamesema kuwa hawataraejea madarasani hadi serikali itakaposhughulikia maslahi yao huku […]

WATU 7 WAKAMATWA ELDORET KWA KUHUSISHWA NA ULAGHAI

Polisi mjini Eldoret wamewatia mbaroni washukiwa saba wanaohusishwa na ulaghai ya kuajiri watu wanaotafuta ajira nje ya nchi katika eneo hilo. Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Uasin Gishu Benjamin Mwanthi amesema washukiwa hao walikamatwa katika afisi kadhaa ambapo wanahudumu ndani ya mji huo. Timu za usalama bado zinaendeleza msako mkali ili kuwakamata washukiwa zaidi […]

WABUNGE KUWA NA UAMUZI WA MWISHO KUHUSU WAKENYA WALIOPEWA MSAMAHA WA USHURU KATIKA MSWADA MPYA

Wabunge watakuwa na uamuzi wa mwisho katika kubainisha ni watu gani au kampuni gani zitapewa msamaha wa kodi ikiwa mswada mpya utakuwa sheria. Mswada wa Marekebisho wa taratibu za Ushuru, 2024, unalenga kurekebisha Sheria ya Taratibu za Ushuru (Sura ya 469B), kuruhusu wabunge kukagua Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Hazina na Kamishna Mkuu wa […]

SERIKALI YA KAUNTI YA KAKAMEGA YANUNUA DAWA ZA MILIONI SITA

Ni afueni kwa wagonjwa na wakaazi wa kaunti ya kakamega baada ya Serikali ya kaunti hiyo kununua dawa za kima cha shilingi milioni sita za hosipitali kuu ya kaunti hiyo. Gavana wa kaunti Hiyo Fernandez Barasa akitoa onyo kali kwa wasimamizi wa vituo vya afya vya kaunti hiyo dhidi ya kuwatuma wagonjwa kununua dawa kwingine […]

WAZIRI WA AFYA KAUNTI YA TRANSNZOIA AWATAKA VIONGOZI KUTOINGIZA SIASA KATIKA MASWALA YA AFYA

Waziri wa afya wa kaunti ya Transnzoia Sam Ojwang ametoa wito kwa viongozi wa kaunti hiyo kutoingiza siasa katika swala la afya na badala yake kushiriki mazungumzo na uongozi wa kaunti ili kujboresha sekta hiyo. Kwa mujibu wa Ojwang kushirikian kutahakikiksha kwamba mamlaka ya kusambaza dawa na vifaa vya matibabu KEMSA inasambaza dawa katika vituo […]

KUPPET YAKIUKA AGIZO LA MAHAKAMA LA KUSITISHA MGOMO

Muungano wa walimu wa sekondari na vyuo vya kadri KUPPET umeapa kuendeleza mgomo wao hadi serikali itakapotekeleza malalamishi yao yote licha ya mahakama ya leba kuwaagiza kusitisha mgomo na kurejea kazini hadi kesi iliyowasilishwa na tume ya kuwaajiri walimu TSC itakaposikilizwa na kuamuliwa. Mahakama ya leba imekitaka chama cha KUPPET kuwasilisha majibu ya kesi dhidi […]

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA MASHIRIKA YA KIMATAIFA KUJENGA KIWANDA CHA NUCLEAR

Waziri wa nishati Opiyo Wandayi amefichua kuwa serikali ya kitaifa inalenga kutafuta ushirikiano katika hazima ya kujenga kiwanda cha Nuclear katika muda wa miaka kumi. Kwa mujibu wa wandayi Kenya itashirikiana na mashirika na washirika wa kimataifa ili kuhakikisha taifa lin azingatia viwango vya juu vya usalama na utayari wa viwanda. Imetayarishwa na Janice Marete

MTU MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI YA BARABARA YA MERU-NAIROBI

Mtu mmoja ameaga dunia eneo la Kajiunduthi kaunti ya Tharaka Nithi kufuatia ajaliiliyotokea katika barabara kuu ya Meru-Nairobi. Ajali hiyo imehusisha malori m awili na gari moja la kibinafsi huku walioshuihudia ajali hiyo wakisema kuwa gari hilo na kibinafsi na lori moja zilikuwa zikielekea upande mmoja wakati ajali hiyo imetokea. Majeruhi wamekimbizwa katika hosipitali moja eneo hilo. Imetayarishwa […]