TIMU YA CHUO KIKUU CHA PEERLESS KABARAK YAFANIKIWA KUFIKA FAINALI KATIKA MECHI ZA KUSF

Timu za michezo za Chuo Kikuu cha Kabarak ziliibuka kidedea wikendi katika michezo ya Shirikisho la Michezo la Vyuo Vikuu vya Kenya (KUSF) iliyoandaliwa katika Chuo Kikuu cha Laikipia, na kupata nafasi katika mashindano yajayo ya kitaifa licha ya kusitishwa ghafla kwa mashindano hayo kwa sababu ya usalama. Katika kategoria ya mpira wa vikapu ya […]

SIJAKUWA NA MSAIDIZI, RAIS RUTO

Nimekosa wa kunisaidia kuwaeleza wakenya kuhusu miradi ya serikali na hivyo kuwa changamoto kuu katika serikali yangu kwa kipindi cha miaka 2 iliyopita. Ni usemi wake Rais William Ruto akizungumza wakati wa kuapishwa kwa naibu rais wa tatu wa Kenya Kithure Kindiki katika ukumbi wa mikutano KICC jijini Nairobi. Kwa mujibu wa Rais, Kindiki ana […]

MAUAJI YA KIJINSIA: RUTO ATAOA AMRI

Katika juhudi za kukabili visa vya mauaji dhidi ya jinsia ya kike ambavyo vimeongezeka nchini na kuzua hofu, Rais William Ruto amehimiza ushirikiano wa wakenya Wote katika kuwakabili wahusika wa mauaji hayo. Akikiri ongezeko la mauaji dhidi ya wanawake na wasichana, Rais ameiagiza idara ya upelelezi DCI na idara ya usalama kwa jumla kuhakikisha wahusika […]

MECHI YA REAL MADRID YAHAIRISHWA KUFATIA MAFURIKO

Mechi ya Real Madrid ya ugenini dhidi ya Valencia katika La Liga wikendi hii iliahirishwa siku ya Alhamisi na shirikisho la soka la Uhispania kutokana na mafuriko yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 95. Mechi ya Villarreal ya nyumbani dhidi ya Rayo Vallecano pia ilisitishwa baada ya mafuriko makubwa yaliyotokea mashariki mwa Uhispania. La Liga […]

AMONDE AONYA KIKOSI CHAKE KISILEGEZE KAMBA

Nahodha wa zamani wa Kenya Sevens Andrew Amonde ameonya kikosi chake cha Shujaa kutarajia majaribio makali wakati Msururu mpya wa Raga ya Dunia ya Saba itakapoanza mwishoni mwa mwezi huu mjini Dubai. Amonde anasema timu nyingi duniani zimeimarika na hivyo basi hitaji la timu ya taifa kuimarika wanaporejea katika hadhi yao ya msingi. Shujaa wanarejea […]

EQUITY HAWKS YALAMBISHWA KIVUMBI

Mabingwa watetezi wa Mamlaka ya Bandari ya Kenya (KPA) walipata ushindi wa 80-63 dhidi ya Equity Hawks na kuingia nusu-fainali ya Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Wanawake ya FIBA ​​Kanda ya Tano ya kufuzu kwa Afrika katika uwanja wa Amaan Indoor Arena nchini Tanzania. KPA pamoja na timu nyingine tatu zilizofuzu kwa nusu fainali […]

LIGI YA WANAWAKE YANOGA

Mabingwa wa zamani wa Ligi ya Kitaifa ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Wavu nchini Kenya Pipeline waliwazaba wapinzani wao Kenya Prisons kwa seti 3-2 huku msimu wa 2024/2025 ukiendelea katika uwanja wa Kamukunji kaunti ya Nyeri mnamo Alhamisi. The Oilers ilishinda kirahisi seti ya kwanza baada ya 25-14 kabla ya Prisons kujipanga upya […]

KOCHA OKERE ALAUMU KIKOSI CHAKE KWA MATOKEO MABAYA

Kocha wa Tusker FC, Charles Okere amelaumu matokeo mabaya ya hivi majuzi kwa kukosa umakini wa kutosha, akionya kudorora kwa msimu wa mapema kunaweza kukatiza malengo yao ya kuwania taji la FKF-Premier League. Okere amesema pia alikuwa na wasiwasi juu ya ukosefu wa tabia ya washabuliaji, akitaja mechi mbili walizoongoza 1-0 na 2-0 dhidi ya […]

WABUNGE WAELEZEA IMANI YAO KWA NAIBU WA RAIS MTEULE KITHURE KINDIKI KATIKA JUHUDI ZA KUUNGANISHA TAIFA

Wabunge wa bunge la kitaifa wakiongozwa na mbunge wa Langata Felix Oduor wameeleza matumaini yao kwa naibu war ais mteule kwamba ataunganisha taifa hili. Wabunge hao akiwemo mbunge wa Dagoret kusini John Kiarie na Antony Oluoch wa mathare kaskazini wameeleza kurithishwa kwao na hatua ya rais william Ruto kumteua Kindiki kama naibu wake. Imetayarishwa na Janice Marete