MIMBA ZA MAPEMA CHANGAMOTO KWA SHA BUNGOMA, SERIKALI

Wasichana kujifungua wakiwa katika umri mchanga wa kabla ya miaka 18 imetajwa kuwa changamoto kuu kwa utekelezaji wa mfumo mpya wa usimamizi wa afya SHA katika kaunti ya Bungoma, serikali kuu ikitakiwa kubuni sera zitakazowashughulikia wasichana hao katika kulipia ada za kujifungua. Kulingana na msimamizi wa SHA kwenye kaunti hiyo Martin Kiprop, serikali inazidisha juhudi […]

TIMIZENI AHADI, WALIMU KWA SERIKALI

Huku ikisalia takribani miezi 2 kabla ya masomo ya gredi ya 9 kuanza, muungano wa walimu wa shule za msingi umeitaka serikali kuwaajiri walimu zaidi watakaofanikisha masomo hayo jinsi iliyoahidi. Wakizungumza jijini Mombasa wakati wa kongamano lao la kila mwaka, wlaimu hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Johnson Nzioka wamesema utekelezwaji wa masomo ya sekondari msingi […]

MAGEUZI YATOKOTA, AZIMIO YATANGAZA

Mageuzi yanatarajiwa katika ulingo wa kisiasa nchini hivi karibuni baada ya kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na mwenzake wa DAPK Eugene wamalwa kutangaza kujiondoa kwenye muungano wa Azimio na kubuni muungano tofauti wa upinzani kabla ya mwaka ujao. Kulingana nao, huenda Musyoka akawa kinara wa muungano huo, na kuongeza kuwa lengo lao ni […]

WASIMAMIZI WA KCSE WEBUYE WAONYWA

Katika juhudi za kuimarisha usalama na ubora wa mtihani wa kitaifa KCSE ambao umeanza hii leo, mkurugenzi wa elimu katika eneo bunge la Webuye Mashariki Dkt Paul Rono amewaonya wasimamizi wa mtihani huo dhidi ya ukiukaji wa mwongozo wa baraza la mitihani ya kitaifa KNEC ikiwemo kuwezesha udanganyifu. Rono ametoa onyo hiyo akiwa mjini Webuye […]

MAHAMKAMA YA UPEO YAATHIMISHA MIAKA 12 TANGU KUZINDULIWA NCHINI

Idara ya mahakama inaathimisha miaka 12 tangu kuzinduliwa kwake hasa mahakama ya upeo nchiniKulingana na jaji mkuu Martha Koome mahakama ya upeo imekuwa na nafasi kubwa katika kulinda katiba na vile vile kuhakikisha wakenya wanapata haki. Akitoa hotuba yake katika kongamano la kuathimisha mi9aka 12 linalofanyika katika ikulu ya Nairobi Koome aidha amezungumzia mchango wa […]

KIPSANG: KILA LA HERI WATAHINIWA WA KSCE

Katibu katika wizara ya elimu Belio Kipsang amewahakikishia watahiniwa wa KCSE usalama wao hawa wle ambao wako katika maeneo yanayoshuhudia utovu wa usalama. Kulingana na Kipsang tayari vitengo mbali mbali vya idar ya usalama vimejitolea kuhakikisha usama wa wanafunzi unadumishwa huku akiwatakia wanafunzi wote kote nchini kila la heri katika mitihani yao. Imetayarishwa na Janice Marete

VIONGOZI WA KAUNTI YA BUSIA WAAGIZWA KUFIKA MBELE YA EACC KUJIBU MASWALI KUHUSU KUAJIRIWA KWAO

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imewaagiza wakurugenzi na manaibu wakurugenzi 39 katika idara mbalimbali za Serikali ya Kaunti ya Busia kufika mbele yake kuanzia leo jumatatu ili kuhojiwa kuhusiana na makosa ya uajiri. Katika taarifa wakurugenzi hao wametakiwa kufika mbele ya maafisa wa EACC mjini Bungoma kibinafsi ili kuangazia jinsi walivyoajiriwa. Hii […]

MAN-U WATOA SARE YA 1-1DHIDI YA CHELSEA

Bao la Moises Caicedo la dakika ya 74 lilifuta bao la kwanza lake Brunoi Fernandez kunako dakika ya 70 kutoka eneo la Hatari. Bao hilo liliinyima Manchester United ushindi katika mechi yao ya kwanza ya Premier League tangu kumtimua kwa Erik ten Hag huku Chelsea ikiambulia sare ya 1-1. Matokeo hayo yalimyima meneja wa united […]

SHEILA CHEPKIRUI AIBUKA KIDEDEA KWA OBIRI KUWANIA TAJI LA NEW YORK CITY MARATHON

Mwanariadha wa Kenya Sheila Chepkirui alishinda taji la New York Marathon kwa wanawake katika mbio zake za kwanza jana Jumapili, na kutwaa taji hilo katika muda wa saa mbili, dakika 24 na sekunde 35.Hellen Obiri, mshindi wa New York Marathon 2023 na mshindi wa medali ya shaba katika Olimpiki, alikuwa sekunde 14 nyuma katika nafasi […]

WAZIRI OGAMBA AONYA WANAOJARIBU KUDANGANYA MTIHANI WAKATI KCSE INAENDELEA

Waziri wa Elimu Julius Ogamba ametoa onyo kali kwa yeyote anayenuia kudhoofisha uaminifu wa mtihani wa Kidato cha Nne (KCSE) ambao unaendelea kote nchini. Jumla ya watahiniwa 965,501 wamejiandikisha kwa mtihani wa mwaka huu katika vituo 10,754 nchini kote na kulingana na Waziri, wale watakaopatikana wakijihusisha na udanganyifu hawatasamehewa. Ogamba alithibitisha kuwa karatasi zote za […]