TALAAM KUSALIA NDANI KWA SIKU 15

Ocs wa kituo cha polisi cha central Samson Talam atasalia kizuizini kwa muda wa siku 15 ili kutoa nafasi ya kukamilishwa kwa uchunguzi katika kifo tata cha mwalimu Albert Ojwang. Katika uamuzi uliotolewa na hakimu Benmark Ekhubi mahakama imeridhishwa na sababu zilizotolewa na upande wa mashtaka za kutaka azuiliwe. Uamuzi huo umechochewa na hatua ya […]

KNH ILIPOKEA MAJERUHI 16 WA MAANDAMANO

Hospitali ya kenyatta ilipokea majeruhi 16 kufuatia maandamano ya hapo jana hapa Nairobi 7 wakilazwa na wengine 9 wakitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Katika mkao na wana habari Daktari mkuu wa upasuaji katika hospitali ya Kenyatta Dr William Sigilai ameelezea hali ya mchuuzi aliyepigwa risasi na polisi na kusema amefanyiwa upasuaji ambapo waliondoa risasi na […]

INZAGHI AWAPUZULIA MBALI WAKOSOAJI

Kocha wa zamani wa Inter Milan Simone Inzaghi amepuuzilia mbali ukosoaji wake kuhusu namna alivyohamia klabu ya Al-Hilal ya Saudia. Inzaghi anaanza kuinoa klabu yake mpya kwa mara ya kwanza Jumatano watakapomenyana na Real Madrid katika Kombe la Dunia la Vilabu huko Miami. Afisa mkuu mtendaji wa Al-Hilal Esteve Calzada aliambia BBC Jumatano kwamba hatua […]

LEVY APIGIA UPATO TOTTENHAM KUCHUKUA LIGI MSIMU MPYA

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy alisema hajutii kumwajiri Ange Postecoglou huku akitetea uamuzi wa kumfukuza kocha huyo raia wa Australia. Postecoglou aliiongoza Spurs kutwaa taji lao la kwanza kwa miaka 17 kwa kushinda Ligi ya Europa mwezi uliopita. Hata hivyo, hiyo haikutosha kuokoa kibarua chake baada ya kumaliza katika nafasi ya 17 kwenye Premier League. […]

OJWANG AREJEA KIKOSINI

Mchezaji wa Nakuru RFC Chrisant Ojwang amerejea katika timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba saba, miezi saba baada ya kufanyiwa upasuaji kufuatia jeraha baya alilopata wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya HSBC World Rugby Sevens huko Dubai. Ojwang alikuwa katika hali nzuri kabla ya kupata jeraha baya lililomweka nje kwa msimu mzima. Atakuwa […]

MANCHESTER UNITED KUVAANA NA ASENALI KATIKA MCHEZO WA UFUNGUZI

Liverpool wataanza kutetea taji lao la Ligi ya Premia wakiwa nyumbani dhidi ya Bournemouth Ijumaa, Agosti 15 huku Arsenal wakimenyana na Manchester United katika mchuano mkali wikendi ya ufunguzi. Mabingwa wa Arne Slot wana nafasi ya kupata alama za kwanza za msimu mpya huko Anfield wanapozindua kampeni ya 2025/26. Kufuatia mchezo wa Bournemouth wana mechi […]

KUMBUKUMBU ZA WAIRIMU

Mwalimu Caroline Wairimu Kihurani, aliyefariki jijini Nairobi wiki jana, amesherehekewa kwa jukumu alilocheza kama mmoja wa wasanii wa kike waanzilishi wa karate nchini Kenya. Wairimu aliweka historia kama mwanamke wa kwanza kuwakilisha nchi katika Mashindano ya Dunia ya Taekwondo mwaka wa 1997 huko Hong Kong, kando na kuwa mshiriki wa pekee mwanamke katika Shirikisho la […]

KENYA KUANDAA MASHINDANO YA PARA VOLLEYBALL

Kenya inajiandaa kuandaa Mashindano maarufu ya Africa Para Volleyball kwa mara ya kwanza kabisa, yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Julai 1 hadi 10, 2025, katika Ukumbi wa Michezo wa Moi, Kasarani. Tukio hilo la kihistoria linaashiria hatua muhimu kwa nchi kwani haliangazii tu kujitolea kwa Kenya katika michezo-jumuishi bali pia kufuzu kwa Mashindano ya Dunia ya Volleyball […]

LSK YATAKA AFISA ALIYEKUWA NA ‘MUUAJI’ AKAMATWE

Chama cha wanasheria nchini LSK kinashinikiza kukamatwa kwa afisa wa polisi aliyekuwa Pamoja na afisa anayesemaekana kukamatwa baada ya kumpiga risasi na kumjeruhi vibaya mchuuzi katikati mwa jiji la Nairobi hapo jana. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio, rais wa LSK Faith Odhiambo, amesisitiza kuwa wawili hao walikuwa wakishirikiana, na hivyo wote wanafaa kukamatwa […]

MZOZO WA NYAMIRA WAPATA DAWA

Hatimaye mzozo wa uongozi kwa kipindi cha zaidi ya miezi 10 katika bunge la kaunti ya Nyamira umeonekana kufikia kikomo baada ya Thaddeus Nyabara kuapishwa rasmi kuwa spika mpya wa bunge hilo. Wakati uo huo, Duke Onyari amekabidhiwa jukumu la kusimamia afisi ya karani wa bunge hilo. Nyabara abnachukua uongozi huo baada ya aliyekiwa spika […]