RUTO AAGIZA BUNDUKI HARAMU ZISALIMISHWE TRANS MARA

Hatimaye Rais William Ruto amevunja kimya chake kuhusu machafuko ya kikoo katika eneo la Transmara South na Transmara West kaunti ya Narok na kuwaamrisha wakazi walio na bunduki haramu kuzisalimisha mara moja. Akitoa agizo hilo, Rais Ruto ameapa kurejesha utulivu katika maeneo hayo ambayo yamekumbwa na mzozo baina ya koo mbali mbali na kusambaratisha masomo […]

REGRAGUI ACHUKUA TAHADHARI DHIDI YA HAKIMI AFCON

Kocha wa Morocco Walid Regragui amesema ataendelea kuwa mwangalifu sana katikamatumizi ya beki nyota Achraf Hakimi kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON), huku mchezaji huyo wa Paris Saint-Germain akiendelea kupona jeraha la kifundocha mguu. Regragui amedokeza kuwa Hakimi alikuwa tayari kucheza kabla ya mechi ya ufunguzi dhidiya Comoros, lakini hatimaye nahodha huyo wa […]

GSU, PIPELINE WATAWALA MASHINDANO YA KIPCHUMBA KARORI

Mabingwa wa mashindano ya Kipchumba Karori walitunukiwa Jumapili, Desemba 21, 2025,pazia liliposhushwa katika toleo la pili la mashindano hayo ya kimataifa.Timu ya wanaume ya General Service Unit (GSU) na Kenya Pipeline Ladies zilitwaaubingwa, zikiendeleza ubabe wao katika soka la wavu la ngazi ya juu nchini.Pande zote mbili zilizoshinda ziliondoka na kitita cha Shilingi milioni moja […]

AFC LEOPARDS TORONTO WANG’ARA CANADA

Kadri Canada inavyozidisha maandalizi ya kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la FIFA2026 katika miji ya Toronto na Vancouver, hamasa ya soka inaendelea kushika kasi kotenchini humo, ikihusisha jamii, mashindano na timu zinazoibukia.Wakiwa miongoni mwa wanaonufaika na msisimko huo ni AFC Leopards Toronto FC,ambao walimaliza nafasi ya pili katika toleo la tatu la mashindano ya […]

NAIROBI UNITED YAKASHIFU GHASIA ZILIZOSITISHA MECHI DHIDI YA GOR MAHIA

Klabu ya Nairobi United inayoshiriki Ligi Kuu ya FKF imezungumza baada ya vuruguzilizozuka jukwaani na kusababisha mechi yao ya nyumbani dhidi ya Gor Mahia kusitishwakabla ya kumalizika jana.Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wao wa Facebook, Nairobi United imeelezamasikitiko yake makubwa kufuatia tukio hilo na kutuma pole kwa mashabiki wotewalioathirika na makabiliano hayo.Mechi hiyo iliyopigwa katika […]

GHARAMA, MAPUNGUFU YA UJUZI YAASHIRIA UZITO KWENYE SEKTA YA UJENZI

Sekta ya ujenzi nchini inakabiliwa na shinikizo kubwa kutokana na kupanda kwa gharama ya vifaa vya matumizi, uhaba wa ujuzi na utumiaji polepole wa zana za kidijitali, masuala ambayo yametawala mijadala katika toleo la nane la Big 5 Construct Kenya, ambalo limevutia wataalamu 9,637 wa sekta hiyo jijini Nairobi. Licha ya idadi kubwa ya washiriki kuashiria mahitaji endelevu […]

UNITED WATAWANYWA NA VILLA

Aston Villa waliimarisha azma yao ya kutwaa taji la Ligi kuu nchini Uingereza EPL baada ya kuwadhalilisha Manchester United kwa kichapo cha mabao 2-1, na kudhoofisha juhudi za United kuingia top 4. Vijana hao wa Unai Emery walichukua uongozi kupitia kwa Morgan Rodgers, ila makosa ya beki Matt Cash yakamzawadi Matheus Cunha nafasi ya kusawazisha […]

AFCON KUFANYIWA MAGEUZI, CAF

Soka la bara Afrika imeratibiwa kufanyiwa marekebisho makubwa, ikiwemo kubuniwa kwa dimba la African Nations League na kubadilishwa kwa dimba la AFCON ambalo litakuwa likiandaliwa kila baada ya miaka 4 tofauti na miaka 2 ya sasa. Katika taarifa kwa wanahabari baada ya mkutano na wadau, Rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF Dakta Patrice […]

MOROCCO WAANZA AFCON KWA USHINDI

Dimba la mataifa bingwa barani Afrika AFCON 2025 ilianza rasmi usiku wa kuamkia leo nchini Morocco huku wenyeji wa dimba hilo Morocco wakifungua kampeni yao ya kusaka ubingwa wa pili wa AFCON kwa ushindi, wakiinyuga Comoros mabao 2-0 katika mechi ambapo Atlas Lions walionyesha utepetevu ambao huenda ukawa kikwazo katika safari yao. Morocco walipoteza mkwaju […]

TUSKER WAWAROVYWA APS BOMET, GOR-UNITED KUSUBIRI

Kamati ya ligi na ushindani chini ya shirikisho la FKF inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu mechi iliyositishwa kati ya Gor Mahia na Nairobi United baada ya mashabiki kurusha vifaa uwanjani katika kipindi cha pili na kulazimu wasimamizi kuisitisha. Kizaazaa hicho kilitokea mechi hiyo iliyokuwa imesubiriwa kwa hamu ikiwa bao 1-1 katika dakika ya 58, wasimamizi wakisema […]