KUCO YALAUMU SERIKALI KUHUSU MGOMO WAO

Katibu mkuu wa chama cha maafisa wa kliniki KUCO George Gibore, amesema serikali haijakuwa tayari kumaliza mgomo wa maafisa hao na kwamba imekuwa ikipuuza matakwa yao. Akizungumza mjini Kisii amesema licha yao kujitolea kushiriki mazungumzo ya kurejea kazini, magavana wamekuwa wamekuwa wakitoa vijisababu. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

OMTATAH MAHAKAMANI KUHUSU WADHIFA WA CAS

Seneta wa Busia Okiya Omtatah na Wakenya wengine watatu wameelekea mahakamni kuishtaki serikali wakitaka kuondolewa kabisa kwa wadhifa wa makatibu waandamizi yaani CAS. Kwenye kesi hiyo ambapo washtakiwa ni mwaansheria mkuu, tume ya huduma za umma PSC na tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi wa umma SRC, walalamishi wanahoji kuwa afisi hiyo sawa na ile […]

NYORO: LISHE SHULENI INGALIPO

Mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa Ndindi Nyoro, amewahakikishia Wakenya kwamba mpango wa lishe shuleni ungalipo na kwamba serikali imetenga shilingi bilioni 3 kuwezesha mpango huo katika awamu ya kwanza. Kauli yake imejiri baada ya kubainika kwamba hazina ya kitaifa imeondoa mpango huo kwenye makadirio ya bajeti ya mwaka wa kifedha wa […]

ACHA KUINGIZA SIASA AU UJIUZULU’ MALALA AAMBIA WAZIRI KURIA, MURKOMEN HUKU AKIMWONYA SUDI

Katibu Mkuu wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) Cleophas Malala ametoa tahadhari kwa baadhi ya viongozi mashuhuri wa chama hicho kwa kile amekitaja kuwa ni dharau kwa uongozi wa chama  Aliporejea kutoka taifa la Uchina pamoja na wajumbe wa UDA Malala amebaini kuwa anafahamu kuongezeka kwa tabia ya utovu wa nidhamu ndani ya chama […]

SERIKALI YATANGAZA TAREHE MPYA YA LIKIZO FUPI KWA WANAFUNZI

Wizara ya Elimu imefanya marekebisho ya tarehe za likizo fupi ili kufidia muda wa masomo uliopotea wakati shule zikilazimika kufungwa kutokana na mafuriko. Kufuatia mabadiliko hayo, yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu wa Elimu Dkt Belio Kipsang Jumatano, wanafunzi wa chekechea, shule za msingi na upili wanatarajiwa kuelekea likizo fupi kuanzia 26 hadi 28 Juni mwaka huu. […]

VIONGOZI WA IGAD WAKUTANA NAIROBI KUJADILI NJIA ZA KUKABILI ATHARI ZA UKAME

Wataalamu kutoka sehemu mbali mbali bara la afrika wamekutana jijini Nairobi ili kujadili njia za kukabili athari za ukame katika ukanda wa Afrika Mashariki. Mkutano huo wa siku mbili umehudhuriwa na wataalamu 150 kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD), ili kuimarisha ushirikiano katika kuboresha uwezo wa kukabiliana na maafa […]

KENYA NA CHINA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA UHUSIANO WA CHINA NA AFRIKA UKIONGEZEKA

Ushirikiano wa kibiashara kati ya taifa la kenya na taifa la Uchina umeendelea kuimarika ,serikali ya kitaifa ya kenya imeandaa mkutano wa kiuchumi jijini nairobi kwa kushirikisha wajumbe wa ngazi za juu kutoka mji wa Shenzhen nchini China. Wawakilishi wa karibu ikiwa ni Pamoja na kampuni 100 za hapa nchini na wawakilishi wa Uchina wanaoishi […]

AMUUA JIRANI KWA MADAI YA KUMWITA BABAYE MCHAWI

Polisi katika eneo la nyakatch kaunti ya Kisumu wamemkamata kijana mmoja mwenye umri wa miaka 18 baada ya kudaiwa kumuua Jirani yake kufuatia madai ya kumwita babaye mchawi Babake mshukiwa ayejulikana kwa jina Valentine Ochieng aliuliwa badae na umma uliojawa na ghadhabu na nyumba nne pia zinazodaiwa kuwa za mshukiwa pia ziliteketezwa Mwili wa marehemu […]

CRISTIANO RONALDO AVUNJA REKODI YA KUFUNGA MABAO MENGI 

Cristiano Ronaldo alivunja rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika msimu mmoja ndani ya ligi ya Saudia baada ya kufikisha magoli 35. Nyota huyo  wa zamani wa Real Madrid na Manchester United alifunga bao la kuongoza kipindi cha kwanza na tena dakika ya 69 kwa kichwa huku Al Nassr ikiilaza Al Ittihad 4-2 nyumbani siku […]

KIKOSI CHA MPIRA WA VIKAPU CHACHAGULIWA

Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Kenya limetangaza kikosi cha muda kwa ajili ya mchujo wa awali wa ​​Afrobasket Zone U-18 unaotarajiwa kufanyika Kampala, Uganda kuanzia Juni 9–14, 2024. Kikosi hicho kinajumuisha wanariadha wachanga wenye talanta kutoka shule mbalimbali kote nchini Kenya. Timu za wavulana na wasichana zitapitia mafunzo ya makazi jijini Nairobi kuanzia Juni […]