LISHE HATARI YAWAUA 4 KITUI

Polisi katika eneo la Kyuso kaunti ya Kitui wanachunguza kisa ambapo watu 4 kutoka Kijiji cha Nganda wamefariki baada ya kula chakula kinachoshukiwa kuwa kibovu. Akithibitisha vifo hivyo, OCPD wa Kyuso Edwin Otieno, amesema waathiriwa walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wamekutana nyumbani wka mkazi mmoja eneo hilo ambako walishiriki chakula cha Pamoja, na kisha wakaanza […]

SERIKALI: REJESHENI MITUNGI YA CYANIDE

Wizara ya afya imetoa tahadhari na kuwataka watu ambao huedna walichuku mitungi ya kemikali hatari ya Sodium Cyanide wakati wa ajali iliyotokea jana kwenye barabara eneo la kati ya Westlands na Limuru kuirejesha. Katika taarifa ya hivi punde kuhusu ajali hiyo, katibu mkuu katika wizara hiyo Mary Muthoni amesema maafisa wa wizara hiyo wamefanikiwa kuiondoa […]

ELIJAH OBEBO AMEAPISHWA KAMA NAIBU GAVANA WA KAUNTI YA KISII

Elijah Obebo ameapishwa kuwa naibu gavana mpya wa kaunti ya Kisii Kiti cha Naibu Gavana wa Kisii kiliachwa wazi mapema mwaka huu kufuatia kutimuliwa kwa Robert Monda mwezi Februari kwa matumizi mabaya ya afisi, kukiuka katiba na utovu wa nidhamu uliokithiri. Gavana Simba Arati mnamo Machi 2024, alimteua Elijah Obebo kwa kukaguliwa na kuidhinishwa na […]

OMTATAH AWAKOSOA VIONGOZI WANAOFUFUA SIMULIZI ZA KIKABILA

Seneta wa Busia Okiya Omtatah ambaye pia ni mkwanaharakati wa kutetea haki za binadamu amekashifu baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao kulingana naye wanajaribu kufufua simulizi za kikabila za mfumo wa kisiasa wa zamani wenye sifa ya ukabila. Katika taarifa kwenye mtandao wa X, seneta huyo amesema kuwa nchi haipaswi kamwe kurudi nyuma kwa siku […]

MWANAMUME MWENYE UMRI WA MIAKA 35 AUAWA KWA KUPIGWA RISASI ISIOLO

Maafisa wa idara ya upelelezi DCI wanachunguza mauaji ya mwanamume mwenye umri wa miaka 35 katika nyumba yake eneo la Aremet, Kaunti ya Isiolo. Mwili wa Lonyiet Lodukai umepatikana ukiwa kwenye kichaka karibu na Shule ya Msingi ya Aremet katika eneo dogo la Aremet. Maafisa wa polisi walitembelea eneo la tukio ambapo wamebaini kuwa marehemu […]

VIONGOZI WA MERU WAMTAKA MALALA KUJIEPUSHA NA MASWALA YA KAUNTI YA MERU

Baadhi ya viongozi wa kaunti ya Meru wamemsuta katibu mkuu wa chama cha UDA Cleophus Malala kwa kumlaumi naibu kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya Meru Ziporah Kinya kwa hatua yake ya kuwasilisha bungeni mswada wa kumbandua mamlakani gavana wa kaunti hiyo kawira mwangaza. Wakiongozwa na seneta wa kaunti hiyo Kathuri Murungi viongozi […]

SINA IMANI NA KALONZO; JOHN MBADI

Mwenyekiti wa chama cha ODM John Mbadi amesema kuwa hana imani na kiongozi wa chama cha wiper Kalonzo Musyoka akitetea haja ya kufanyika mazungumzo na serikali ya kenya Kwanza. Mbadi vile vile amemsuta rais Mtaaafu Uhuru Kenyatta kwa madai kwamba alikuwa na nafasi wazi kumsaidia kiongozi wa ODM Raila Odinga ila hilo halikufanyika. Imetayarishwa na Janice […]

CBC INA DOSARI, IONDOE – GAVANA NATEMBEYA

Gavana wa Trans-Nzoia George Natembeya amependekeza kufutiliwa mbali kwa Mtaala wa elimu Unaozingatia Umahiri CBC huku akiibua wasiwasi kuhusu athari zake kwa mustakabali wa wanafunzi. Natembeya amesema wazazi, wanafunzi na wadau wengine wa elimu wanaonekana kutoelewa mtaala huo wa CBC. Imetayarishwa na Janice Marete

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUMKATA JIRANI YAKE MKONO

Mvulana mwenye umri wa miaka 17 anauguza majeraha katika hospitali ya rufaa ya Kaunti ya Siaya ambapo alikimbizwa baada ya kuokolewa kutoka mikononi mwa umati wenye hasira uliotaka kumuua katika kijiji cha Mahaya Kaunti ya Siaya. Mtoto huyo aliokolewa na polisi baada ya wananchi kumshukia kwa madai ya kushambulia na kumkata mkono jirani yake Mariko […]

WAKFU WA FORD FOUNDATION WASEMEKANA KUTOFAFANUA UFATHILI WAKE

Katibu katika wizara ya mashauri ya kigeni Korir Singoi ametoa taarifa kwamba wakfu wa FORD FOUNDATION haujatoa ufafanuzi unaohitajika kufuatia madai yaliytoibuliwa kwamba wakfu huo unafathili maandamano ya humu nchini. Singoi aidha amefichua kuwa licha ya serikali kupitia wizara ya mashauri ya kigeni kuandikia wakfu huo barua likitaka kutoa maelezo zaidi kuhusu ufathili wake wa […]