ISRAEL WATUA PARIS

Wawakilishi wa Olimpiki wa Israel walisafiri kwa ndege kuelekea Paris siku ya Jumatatu huku kikosi cha Palestina kikitoa wito wa kuwapiga marufuku wachezaji wa Israel kutokana na vita vya Gaza. Michezo hiyo itaanza Ijumaa hi dhidi ya hali ya wasiwasi mkubwa wa usalama na kuongezeka kwa hasira ya kimataifa juu ya idadi ya vifo na […]

WANA BUNDUKI WAKO MBIONI KUMSAJILI RICCARDO

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anasema klabu hiyo inajaribu kuimarisha “nafasi fulani” huku wakikaribia kumsajili mlinzi wa Italia Riccardo Calafiori. Akizungumza mjini Los Angeles mwanzoni mwa ziara ya mechi tatu za Arsenal nchini Marekani dhidi ya Bournemouth, Manchester United na Liverpool, Arteta aliwaambia waandishi wa habari kuwa “hakuna jipya” kuhusu mkataba wa kijana huyo wa […]

AMADOU AJIUNGA NA VILLA

Aston Villa wamemsajili kiungo Amadou Onana kutoka Everton kwa mkataba wa £50m. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alicheza kila dakika ya kampeni ya Ubelgiji ya Euro 2024 na sasa ana fursa ya kuiwakilisha Villa kwenye Ligi ya Mabingwa ulaya ya msimu ujao. Onana alijiunga na Everton kutoka Lille kwa £33m mwaka 2022 na […]

TUTAOGELEA KWA USHINDI KULE PARIS

Kocha wa Kenya wa kuogelea Fakry Mansoor na imani kua wachezaji wake Ridwan Abubakar na Maria Brunlehner watafuzu kwa nusu fainali ya Michezo ya Olimpiki ya Paris. Akizungumza Alhamisi, alisema Abubakar amezidisha maandalizi yake kwa kushiriki katika mashindano ya vyuo vikuu nchini Uingereza kabla ya shughuli ya ziada katika mji mkuu wa Ufaransa. Ridhwan Abubakar, […]

WERE AGURA ZESCO

Mchezaji wa kimataifa wa Kenya, Zescowere ameachana na vigogo wa Zambia Zesco United FC baada ya kumaliza mkataba wake. Were ambaye alikuwa kwenye awamu yake ya pili na Zesco alikuwa sehemu ya orodha ya wachezaji 10 ambayo ilitolewa na klabu hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Zesco Charles Kalala alithibitisha kuondoka kwa Were pamoja na mshambuliaji wa […]

TUWE NA SUBIRA ASEMA BARRY

Mkurugenzi Mtendaji wa FKF Barry Otieno amewataka wadau wa soka kuwa na subira, wanapofanya makubaliano na Wizara ya Elimu ambayo itawawezesha Emerging Starlets kufanya mitihani yao ya KCSE na kucheza Kombe la Dunia la FIFA la U17 la 2024 lijalo. Mashindano hayo yatakayoandaliwa kwa Jamhuri ya Dominika tarehe 16 Oktoba 2024 – 3 Novemba 2024 […]

POLISI WANASA PIKIPIKI 59 ZILIZOIBWA

Polisi mjini Eldoret wamewakamata watu wanne akiwemo mmiliki wa karakana baada ya kuwanasa na pikipiki 59 na sehemu 35 za injini zilizokuwa zimeibwa kutoka kwa wahudumu wa bodaboda katika kaunti ya Uasin Gishu. Akiwahutubia wanahabari katika kituo cha polisi cha Central mjini humo, kamanda wa polisi Benjamin Mwathi amesema pikipiki hizo zimenaswa katika karakana eneo […]

VITAMBULISHO VYA WAKENYA KUHARIBIKA BAADA YA MIAKA 10

Wakenya watahitajika kubadilisha vitambulisho vyao kila baada ya miaka 10, katibu katika idara ya uhamiaji Julius Bitok akisema ilivyo kwa kadi za ATM, kijipande cha silikoni ambacho kinawekwa ndani ya vitambulisho hivyo mpya huharibika baada ya muda huo wa miaka 10. Katika taarifa kwa wanahabari, Bitok ametetea hatua ya serikali kuleta vitambulisho vya kidijitali, akisema […]

WALUKE AWAONYA WAKAZI DHIDI YA KUANDAMANA

Mbunge wa Sirisia John Waluke amekashifu vikali mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayodaiwa kufadhili maandamano yanaoendeshwa na vijana wa kizazi cha Gen z akihoji kuwa maandamano hayo yanalemaza maendeleo kando na kuvuruga amani. Akihutubu kwenye hafla moja eneo la sirisia, Waluke amesema maandamano hayo yametekwa na wahuni wanayotumia fursa hiyo kutekeleza uhalifu. Wakati uo huo, Waluke […]

MRATIBU AYAKANA MASHIRIKA

Mwenyekiti wa mamlaka ya kudhibiti mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na kijamii Mwambu Mabonga amesema mashirika 16 yaliyohusishwa na ufadhili wa maandamano nchini yanachunguzwa, akisema ni mashirika matatu pekee kati ya 16 hayo ndiyo yamesajiliwa na mamlaka hiyo. Katika kikao na wanahabari jijini Nairobi, Mabonga amesema faili za mashirika hayo zimewasilishwa kwa idara ya ujasusi DCI […]