WAKAAZI WA MIGORI WALALAMIKIA KUMWAGIKA KWA KEMIKALI ZENYE SUMU KUTOKA KWA MIMEA INAYOSAFISHA DHAHABU

Wakaazi wa eneo la Oruba-Siany kaunti ya Migori wameibua wasi wasi wao kufuatia kumwagika kwa kemikali zenye sumu kutoka kwa baadhi ya mitambo ya uchenjuaji dhahabu katika eneo hilo. Wakaazi hao sasa wanatafuta uingiliaji kati wa Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Mazingira (NEMA) huku wakisema wanyama wao wamekufa baada ya kunywa maji yaliyochafuliwa na zebaki […]

INJERA ANA IMANI WATAREJEA KWA KISHINDO

Mchezaji maarufu wa raga ya wachezaji saba wa Kenya, Collins Injera, ameelezea imani na matumaini katika kikosi cha sasa cha vijana cha Shujaa. Injera, anayejulikana kwa uwezo wake wa kufunga mabao mengi na mchango mkubwa katika raga ya Kenya, anaamini kuwa timu ya sasa ina talanta na uwezo wa kufanya vyema katika mashindano yajayo. Usaidizi […]

TALANTA YAELEKEA KUKAMILIKA

Ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Talanta jijini Nairobi unaendelea vyema.  Rais William Ruto alikagua maendeleo ya ujenzi Jumanne alasiri na kusema uwanja wa michezo utakamilika kabla ya mwisho wa mwaka ujao tayari kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mnamo 2027. Uwanja huo utatumika kama uwanja kwa baadhi ya mechi za Afcon.   Rais […]

KAYOLE STARLETS WAKO MBIONI KUJIANDAA

Klabu ya Kayole Starlets ya Ligi ya Taifa ya Wanawake (NSL) imeimarisha maandalizi yao ya msimu ujao. Kocha mkuu wa timu hiyo Mary Adhiambo aliangazia lengo kuu la klabu hiyo la kuinua daraja hadi ligi ya daraja la juu, Ligi Kuu ya Wanawake ya Kenya (KWPL). Mbali na mipango yao ya kimkakati, kocha Adhiambo alifichua […]

TUPO TAYARI KWA MSIMU UJAO

3K FC wameongeza maandalizi yao ya kabla ya msimu mpya kabla ya mechi yao ya kwanza katika ligi ya daraja la pili nchini Kenya, National Super League (NSL). Timu hiyo yenye maskani yake Embu ambayo ilipandishwa daraja kutoka Daraja la Kwanza, itakabiliana na mchuano wao mkubwa zaidi katika historia yao changa, lakini kocha mkuu Francis […]

NAKURU YATENGA MILIONI 100 ZA UKARABATI WA BARABARA

Kaunti ya Nakuru imetenga Shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukarabati wa barabara kuu zilizoathiriwa na mvua iliyonyesha hivi majuzi na kusababisha uharibifu mkubwaPesa hizo zitatumika kutunza barabara muhimu katika kata zote 55, huku serikali ikitafuta bajeti ya juu zaidi kukarabati miundombinu hiyo. Mvua kubwa ilinyesha nchini miezi mitatu iliyopita, na kuua makumi ya watu, […]

RAIS MADURO AKIMBIA IKULU

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametoroka kutoka ikulu yake kutokana na maandamano makali ya kupinga uchaguzi wake, waandamanaji wakisafiri kutoka kilomita kadhaa na kutishia kuvamia ikulu hiyo. Mapema leo, vikosi vya usalama vimetumia risasi za mipira na vitoza machozi kuwakabili waandamanaji. Vurugu zimeanza katika jiji kuu la Caracas baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza Maduro […]

DORCAS ODUOR ATEULIWA KUWA MWANASHERIA MKUU

Rais William Ruto amemteua Dorcs Oduor kuwa mwanasheria mkuu ambaye kwa sasa anahudumu kama katibu katika afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma ODPP. Oduor ambaye ni wakili wa mahakama kuu, amewahi kuhudumu kama naibu mkurugenzi katika afisi ya ODPP na mwanasheria wa serikali kwenye afisi hiyo. Uteuzi wake unajiri baada ya Rebecca Miano ambaye […]

MKENYA ATAKA KUFUTILIWA MBALI PENDEKEZO LA ADANI

Mkenya kwa jina Lango Guyo amewasilisha kesi katika mahakama ya Milimani akitaka kusitishwa kwa pendekezo la shirika la Adani Airport kupewa kandarasi ya kuukarabati uwanja wa ndege wa JKIA, akisema zoezi hilo lilifanywa bila kushirikisha wananchi na ukosefu wa uwazi, inavyohitajika kisheria. Kwa mujibu wa Guyo, mchakato mzima wa utoaji wa kandarasi hiyo ulikumbwa na […]

‘MHARIBIFU WA SHEREHE’ AKAMATWA ELDORET

Huku mji wa Eldoret ukijiandaa kupandishwa hadhi na kuwa jiji la tano nchini wiki ijayo, polisi mjini humo wamemkamata mwanamme mmoja aliyenaswa kwenye kamera za siri aking’oa miche iliyokuwa imepandwa kwa matayarisho ya sherehe hizo. Huku lengo la mshukiwa kuharibu miche hiyo halijabainika, baadhi ya wenyeji wanasema kwamba ana akili tahira na anazuiliwa katika kituo […]