KAUNTI YA BARINGO CHINI YA UCHUNGUZI WA SENETI DHIDI YA AKAUNTI 304 ZA BENKI

Bunge limeiagiza Serikali ya Kaunti ya Baringo kutoa stakabadhi zinazoelezea makubaliano kati ya kaunti hiyo, Mdhibiti wa Bajeti na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kuhusu kufunguliwa kwa akaunti 304 za benki kinyume cha sheria. Maseneta walitoa agizo hilo jana Jumatatu Gavana wa Baringo Benjamin Cheboi alipofika mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu Ugatuzi na […]

HAKUNA MPANGO NA ADANI HOLDINGS, MUDAVADI ANASEMA KUHUSU SAKATA YA JKIA

Waziri Mkuu Musalia Mudavadi sasa anasema kuwa serikali haijatia saini makubaliano yoyote na Kampuni ya Adani Airports Holdings Limited kuhusu kuboresha miundombinu ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA). Katika ufafanuzi kuhusu Pendekezo la Kibinafsi (PIP) la kundi hilo, Mudavadi amesema pendekezo la Adani Holdings kwa sasa linashughulikiwa vyema ikiwa ni pamoja […]

MASENGELI ASHIKA USUKANI

Naibu inspekta mkuu katika idara ya polisi wa utawala Gilbert Masengeli ameanza rasmi majukumu yake baada ya kukabidhiwa afisi na mtangulizi wake James Kamau, akiahidi kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria. Akihutubu katika makao makuu ya polisi wa utawala jijini Nairobi waketi wa hafla hiyo, Masengeli amesema jukumu kuu la polisi ni moja tu […]

WAKAAZI MUMIAS WASHUTUMU POLISI

Wakazi wa Mumias Mashariki kaunti ya Kakamega wamewashutumu maafisa ya polisi katika kituo cha polisi cha Shianda kwa madai kwamba maafisa hao wameshindwa kukabili uhalifu eneo hilo. Wakiongozwa na David Wamatsi, wakazi wamewalaumu polisi kwa kukosa kumchukulia hatua mshukiwa wa mauaji ya mkazi mmoja kwa kumgonga na pikipiki yapata miezi miwili iliyopita. Wakazi hao sasa […]

HATUNA UBAYA NA WENZETU, MUNYA

Kinara wa chama cha PNU ambacho ni chama tanzu katika muungano wa Azimio la Umoja Peter Munya, amewataka viongozi wa upinzani walio na nia ya kuingia serikali kufanya hivyo mara moja badala ya kujificha kwenye upinzani. Munya anesema kwamba serikali inahitaji upinzani dhabiti ili kutekeleza wajibu wake na hilo litawezekana tu iwapo upinzani utasalia imara. […]

RAILA AWASILISHA RASMI AZMA YA AUC

Kenya imewasilisha rasmi azam ya kinara wa ODM Raila Odinga kuwania wadhifa wa uwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika AUC kwa Mkuu wa umoja wa Afrika kanda ya mashariki ambaye pia ni Balozi wa Mauritius Dharmraj Busgeeth. Katibu katika wizara ya masuala ya kigeni Korir Sing’oei akiwa amendamana na mwandani wa Odinga Makau Mutua […]

ALIYEKUWA MBUNGE WA EMBU ANASAKWA NA POLISI

Maafisa wa upelelezi wanamsaka aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Kaunti ya Embu baada ya kuhusika katika kisa cha ufyatulianaji risasi katika Mji wa Embu jana Jumapili. Kwa mujibu wa mbunge huyo wa zamani ni mmiliki wa bunduki aliye na leseni. Inasemekana alikuwa na ugomvi na mtu aliyekuwa akifurahiya katika eneo moja la burudani mjini humo […]

SENETA ONYONKA; NAJUA NINACHOKISEMA

Seneta wa kisii Richard Onyoka amerejelea matamshi yake kwamba serikali inapanga kuuza uwanja wa kimataifa wa Ndege JKIA muda mfupi baada ya rais william Ruto kukanusha madai hayo. Onyonka amepuuzilia mbali matamshi ya rais william Ruto huku akidai kuwa ana sababu za kusisitiza madai hayo. Imetayarishwa na Janice Marete

WACHA MCHANGANYIKO

Mechi ya ufunguzi ya olimpiki ya Sudan kusini iligubikwa na makosa ya aibu ya wimbo wa taifa yaliyofanywa na waandaaji siku ya jumapili. Timu hiyo ya afrika ya mpira wa vikapu ilionekana kuchanganyikiwa baada ya wimbo wa sudan kuchezwa walipokuwa wakipanga mstari kabla ya mpambano wao na puerto rico. Mashabiki wa sudan kusini katika uwanja […]

HATUJAKA TAMAA ASEMA WAMBUA

Kocha mkuu wa timu ya raga ya wachezaji saba ya wanaume ya kenya kevin wambua anaamini kwamba timu yake ilikuwa na wakati mzuri wa kustaajabisha katika michezo ya olimpiki ya paris, licha ya kukosa kushinda mechi hata moja hatua ya makundi na hatimaye kumaliza katika nafasi ya tisa kwa jumla. Wambua alikuwa akizungumza baada ya […]