KABRAS WAZIDI KULAMBA SUKARI

Kabras RFC ilishinda mkondo wa christie sevens wa msururu wa kitaifa wa 7s baada ya kuwalaza wenyeji kenya harlequins 17-12 katika fainali jana jumapili. Akizungumza baada ya mechi ya fainali, kocha wa timu ya wachezaji saba wa kabras, felix khaemba alisifu azma ya timu yake kurejea katika njia za ushindi. Kwa upande wake, kocha mkuu […]

TUPO TAYARI KWA OLIMPIKI

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya, malkia strikers, Japheth Munala na naibu rais wa shirikisho la voliboli nchini Paul Bitok wamepigia upato timu hiyo kutamba dhidi ya mabingwa mara mbili wa olimpiki brazil, katika mechi ya ufunguzi ya kundi b katika mashindano ya olimpiki. Imetayarishwa na Janice Marete

BONIFACE MWANGI, WENZAKE WAPEWA DHAMANA

Mwanaharakati Boniface Mwangi na washtakiwa wenza wanne wameachiwa huru kwa dhamana ya shilingi elfu 20 kila mmoja baada ya mahakama ya Milimani kudinda kutoa amri ya kuwazuilia kwa siku 21 jinsi upande wa mashtaka ulivyokuwa umeomba. Watano hao walikamatwa hapo jana katikati mwa jiji nla Nairobi walipokuwa wakiandamana kuadhimisha mwezi mmoja tangu maafa yalipotokea katika […]

GACHAGUA AZUNGUMZIA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

Naibu Rais Rigathi Gachagua amepongeza hatua ya rais William Ruto kuwajumuisha viongozi wa upinzani kwenye baraza jipya la mawaziri, akisema hatua hiyo ni ushindi kwa wakenya wote na wala hakuna aliyepoteza. Akizungumza katika hafla ya mazishi katika kaunti ya Nyandarua, Gachagua amesema eneo la Mlima Kenya limefurahia uteuzi huo kwani uteuzi wa Mercy Wanjau kuwa […]

KESI MAHAKAMANI KUPINGA UTEUZI WA VIGOGO WA ODM

Mwanaharakati Julius Ogogoh kupitia kwa shirika la Human Rights and Justice amewasilisha kesi mahakamani kupinga uteuzi wa wanachama wa ODM ambao ni Wycliffe Oparanya, Opiyo Wandayi, Ali Hassan Joho na John Mbadi katika baraza jipya la mawaziri. Kwenye kesi hiyo, mwanaharakati huyo amesema kwamba uteuzi wa wanne hao utahilafiana na majukumu ya kikatiba yanayohitaji upinzani […]

KNUT SASA YAILILIA SERIKALI

Chama cha kitaifa cha kutetea maslahi ya walimu KNUT kimeitaka serikali kurejesha kima cha shilingi bilioni 10.1 zilizopunguzwa kutoka kwenye bajeti ya tume ya kuwaajiri walimu TSC katika mwaka huu wa kifedha baada ya kutupiliwa mbali kwa mswada wa fedha. Katika taarifa, katibu mkuu wa KNUT Collins Oyuu amelalamika kwamba licha ya TSC kurai kamati […]

POLISI KUONGEZWA BILIONI 29

Wizara ya usalama wa kitaifa imesema kwamba serikali imeongeza mgao wa shilingi bilioni 29.4 kwa idara ya polisi katika mpango wake wa kuboresha mazingira ya utendakazi wa maafisa wa polisi katika kipindi cha miaka 3 ijayo. Kupitia taarifa, wizara hiyo imesema fedha hizo zitatumika kwa ununuzi wa vifaa vya kisasa yakiwemo magari na helikopta kwa […]

BUNGE LA BUNGOMA LAWACHUNGUZA MAWAZIRI WAWILI

Wawakilishi Wadi katika bunge la Kaunti ya Bungoma wakiongozwa na kiongozi wa walio wengi Juma Nyongesa, wameapa kuendeleza uchunguzi dhidi ya Waziri wa Fedha Chrispinus Barasa na Waziri wa Elimu kwenye kaunti nhiyo Benedict Emachar kuhusiana na madai ya matumizi mabaya ya fedha za basari na ‘ufadhili wa kaunti maarufu kama Scholarship ya mwaka wa […]

“HATULIPI HIYO!” BODA BODA WAPINGA ADA

Wahudumumu wa boda boda kaunti ya Nandi wamefanya maandamano kulalamikia kurejeshwa kwa ada ya kuegesha pikipiki mjini Kapsabet, muda mfupi baada ya maafisa wa manispaa ya kaunti hiyo kunasa pikpiki kadhaa ambazo hazikuwa na nembo ya kaunti. Wahudumu hao wameelekea hadi katika za maafisa hao wakitaka kujua sababu ya kunaswa kwa pikipiki za wenzao, licha […]

MAREKANI YAMSUTA RUTO

Waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani Antony Blinken amemtaka Rais William Ruto kuheshimu mchango wa vijana katika maendeleo ya taifa la Kenya, akisisitiza umuhimu wa vijana kuruhisiwa kujieleza kupitia maandamano kisheria. Katika mazungumzo ya simu baina ya wawili hao, Blinken aidha ameponegeza hatua ya Ruto kuiagiza mamlaka huru ya kuchunguza mienendo ya maafisa wa […]