SHINIKIZO JUU YA SHINIKIZO KWA RUTO

Viongozi wa mashirika ya kijamii wamemtaka Rais William Ruto kutekeleza masuala ambayo yemeibuliwa na Wakenya na hasa kupunguza matumizi ya serikali. Wakiongozwa na afisa mkuu wa shirika la Transparency International Irungu Houghton, viongozi hao wamekosoa visa vya utekenyaji nyara vinavyoaminika kutekelezwa na maafisa wa polisi kwa lengo la kuzima sauti zinazopinga serikali. Aidha, wameapa kumshtaki […]

NILIPIGA KURA YA NDIO NA SIOMBI MSAMAHA; ALFRED KIPRONOH MUTAI ASEMA

Mbunge wa Kerosoi kaskazini Alfred Kipronoh Mutai amesema kwamba hataomba msamaha wakati wabunge wengine wanaendelea kuomba musamaha kufuatia hatua yao ya kuunga mkonoi mswada wa fedha 2024. Korosoi ameendelea kukashifu uvamizi na uharibifu uluotekelezwa na waandamanaji katika makaazi ya wabunge wenzake Imetayarishwa na Janice Marete

KWA NINI OMBI LA RAILA LA KUGOMBEA WADHIFA WA MWENYEKITI WA AUC BADO HALIJAWASILISHWA?

Ombi la kinara wa upinzani Raila Odinga kuwania wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) bado halijawasilishwa kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao. Katibu Mkuu wa Masuala ya Kigeni Korir Sing’oei amesema kwamba ombi la Raila bado halijawasilishwa kutokana na machafuko na mkanganyiko ambao umekumba nchini katika muda wa wiki mbili zilizopita.Uwasilishaji […]

WATU 4 WAFARIKI WAKICHIMBA MIGODI YA DHAHABU MOYALE MARSABIT

Watu wanne wamethibitishwa kuaga dunia katika maeneo ya uchimbaji madini ya Hillo kaunti ndogo ya Moyale kaunti ya Marsabit huku mamlaka ikijitahidi kuzima shughuli hiyo haramu ya uchimbaji madini. Naibu Kamishna wa Kaunti ya Moyale Benedict Munyoki amesema kuwa wachimba migodi ambao baadhi yao hawana kibali cha kuchimba migodi walifanikiwa kujipenyeza katika eneo la operesheni […]

GAVANA WA SIAYA JAMES ORENGO AMTAKA RAIS RUTO KUJIUZULU

Gavana wa Siaya James Orengo sasa anamtaka Rais William Ruto kujiuzulu akishikilia kuwa kuna hasira nyingi za umma dhidi ya serikali ya Kenya Kwanza. Kwa mujibu wa Orengo iwapo Rais Ruto angesikiliza hisia za watu nchini, angeweza kujiuzulu kwa sababu Wakenya wamechoshwa na utawala uliopo. Kufuatia kutupiliwa mbali kwa Mswada wa Fedha wa 2024 ambao […]

NIS WALITOA TAARIFA YA KUTOSHA RUTO ASEMA

Rais William Ruto jana Jumapili alipuuzilia mbali madai kwamba Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS) haikutoa taarifa za kutosha za kijasusi kabla ya maandamano yaliyoongozwa na vijana ya kupinga Mswada wa Fedha. Kwa mujibu wa Ruto kulikuwa na ripoti za kutosha za kijasusi kwamba wahalifu walikuwa wakipanga kujipenyeza katika maandamano ya amani ya Jumanne. Ameongeza […]

NITAUNGA RUTO MKONO HADI MWISHO ASEMA GACHAGUA

Naibu Rais Rigathi Gachagua amewataka viongozi wa Kenya Kwanza kushughulikia maswala ambayo yameibuliwa na wananchi kuhusu utawala wa Rais William Ruto. Akizungumza eneo la Kaplong, Kaunti ya Bomet, Naibu Rais amewataka viongozi ambao kulingana naye wameonyesha kiburi na utajiri badala ya kufanya kazi kulingana na manifesto ya Utawala wa Kenya Kwanza. Gachagua ameongeza kuwa uhusiano […]

ITALIA WATABAKIA NA LUCIANO

Luciano Spalletti atasalia kama kocha wa Italia licha ya Azzurri kuondolewa katika michuano ya Euro 2024, mkuu wa soka nchini humo alisema Jumapili. Italia ilitupwa nje ya michuano ya Euro katika hatua ya 16 bora baada ya kuchapwa 2-0 na Uswizi mjini Berlin Jumamosi usiku, lakini utetezi mbaya wa ubingwa haujamgharimu Spalletti kibarua chake. “Mimi […]

UHISIPANIA WAINGIA ROBO FAINALI

Rodri, Fabian Ruiz, Nico Williams na Dani Olmo wote walifunga Uhispania ikitoka nyuma na kuwashinda Georgia mabao 4-1 kwenye Euro 2024 Jumapili na kuandaa hatua ya robo fainali dhidi ya wenyeji Ujerumani. Bao la kujifunga la Robin Le Normand liliwapa Georgia bao la kuongoza katika dakika ya 18 ya mchezo huu wa hatua ya 16 […]

KENYA NDO WASHINDI WA KABADDI

Kenya ilinyakua taji la Ubingwa wa Afrika Kabaddi 2024 Jumamosi jioni baada ya kulaza Uganda 44-23 katika mechi ya mwisho ya msururu huo ulioandaliwa Kasarani. Kenya ilianza mechi kwa nguvu huku James Kamweti akizalisha mashambulizi kadhaa katika nusu ya Uganda na kuiweka Kenya mbele wakati wa mapumziko kwa alama 20-13. Ushindi huo unamaanisha kuwa Kenya […]