MWANGI APANGA TAMASHA UHURU PARK KWA KUHESHIMU WAANDAMANAJI WALIOFARIKI

Mwanaharakati Boniface Mwangi anapanga tamasha la wazi bila malipo katika bustani ya Uhuru Park kuwaenzi waandamanaji wote walioaga dunia kwa kupigwa risasi walipokuwa wakitekeleza haki yao ya kidemokrasia ya kupinga mswada wa fedha. Alipokuwa akishiriki mipango hiyo katika mtandao wa X, Mwangi amesema juhudi za kumfikia Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja zimegonga mwamba. Mwangi ameongeza […]

OTIENDE AMOLLO KUONGOZA MISHENI YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI NCHINI UINGEREZA

Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo ametangaza kuwa ataongoza Misheni ya Waangalizi wa Uchaguzi nchini Uingereza ambayo inatazamiwa leo hii. Amolo amekaribisha fursa ya kuongoza misheni hiyo ambayo inajumuisha majimbo na wilaya 19 zikiwemo Kenya, Malawi, St Lucia, Jimbo la Alderney, New South Wales, Seychelles, Trinidad na Tobago, Bunge la Jimbo la Jersey na Grenada. Nyingine […]

NAIBU RAIS RIGATHI GACHAGUA AWAHAKIKISHIA WAKAAZI WA LAIKIPIA USALAMA

Naibu wa rais Rigathi Gachagua amewataka maafisa wa usalama katika kaunti ya Laikipia kuimarisha usalama katika kaunti hiyo. Kwa mujibu wa Gachagua rais William Ruto amejitolea kutimiza ahadi aliyotoa ya kumaliza utovu wa usalama katika kaunti hiyo ya Laikipia. Ameogeza kuwa serikali imeweka mikakati ya kukomesha visa vya uvamizi wa wanyamapori karibu na mbuga za wanyama. Imetayarishwa […]

“HAKUNA KAZI!” – IDARA YA MAHAKAMA

Idara ya huduma za mahakama JSC imefutilia mbali shughuli za kuwaajiri majaji 11 wa kuhudumu katika mahakama ya rufaa. Katika taarifa, jaji mkuu Martha Koome amesema hatua hiyo ni njia mojawapo ya kubana matumizi ya fedha kwa angalau asimilia 15 ilivyoamriwa na hazina ya kitaifa, na kuongeza kwamba ilivyo kwa sasa hawana uwezo wa kuajiri. […]

RUTO AAGIZA TANGAZO LA SRC KUANGAZIWA

Rais William Ruto ameiagiza hazina ya kitaifa kuangazia upya tangazo la tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi wa umma kutaka kuwapandisha mishahara wafanyakazi wa ngazi ya juu serikalini. Katika taarifa, rais amesema amehimiza idara zote za serikali kuendesha shughuli zao kulingana na hali ya uchumi nchini na kubana matumizi yao baada ya kutupiliwa mbali mswada […]

JALANG’O AOGOPA ‘MTEGO’

Huku hayo yakijri, mbunge wa Lang’ata Felix Odiwour maarufu kama jalang’o, ametaja hatua ya SRC kutaka kuwaongeza mishshara wafanyakazi wa ngazi ya juu serikalini kama mtego hasa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi. Kupitia mitandao ya kijamii, Jalang’o amesema atakataa nyongeza hiyo. Hatua ya SRC tayari imeibua hisia kali miongoni mwa Wakenya, nyongeza ya mishahara […]

KHALWALE: VUNJA BARAZA LA MAWAZIRI

Seneta wa kakamega Boni Khalwale amependekeza kuvunjwa baraza la mawaziri ikiwa ni miongoni mwa masuala anayofaa kuyatekeleza Rais William Ruto kutokana na malalamishi yaliyoibuliwa wakati wa maandamano. Akizungumza bungeni alipokuwa akichangia mjadala, Khalwale ametaka wadhifa wa mkuu wa mawaziri ambao kwa sasa unashikiliwa na Musalia Mudavadi pia kuondolewa. Aidha, amepndekeza kuondolewa kwa nyadhifa zisizo kwenye […]

CHERUIYOT AKUBALIANA NA MAGEUZI SERIKALINI

Kiongozi wa walio wengi katika bunge la seneti Aaron Cheruiyot, amewasilisha bungeni humo hoja ambayo inaunga mjadala ulioanzishwa kufuatia maandamano ya Gen Z ya kufanyika kwa mageuzi katika uongozi serikalini. Akizungumza katika bunge la seneti, Cheruiyot amekiri kuwepo kwa changamoto za ufisadi na maadili katika uongozi ambao umesababisha utendakazi duni na ubadhirifu wa fedha za […]

RAGA YA VIJANA WA CHINI YA MIAKA 20 YACHARAZWA 25-7

Timu ya Kenya ya Raga ya vijana wa chini ya miaka 20 ilianza mashindano ya dunia ya raga ya vijana wa Under 20 kwa kupoteza ambapo walicharazwa mabao 25-7 dhidi ya mabingwa wa zamani Urugwi jana jumanne. Hata hivyo kenya ilifanikiwa kupata tri moja ya kujifariji kupitia kwa michael Wamalwa na ni lazima ishinde mechi […]

UKOMBOZI WA MACHOZI KWA RONALDO KWENYE ‘EURO ZA MWISHO

Ukombozi Wa Machozi Kwa Ronaldo Kwenye ‘Euro Za Mwisho” Mkono wa Jan Oblak ulipopenyeza penalti ya muda wa ziada ya Cristiano Ronaldo kwenye nguzo, ndoto za nguli huyo wa Ureno zilikatizwa kwa muda mfupi. Penalti ya Ronaldo iliokolewa katika muda wa nyongeza na mechi ya hatua ya 16-bora bila bao, lakini dakika 15 baadaye alipanda […]