MIMI NA WANDANI WANGU TUNALENGWA- GACHAGUA

Naibu Rais Rigathi Gachagua amedai kwamba afisa wa zamani wa idara ya ujasusi wa kitaifa NIS ambaye aliajiriwa na Gachagua baada ya kutimuliwa na idara hiyo alipigwa risasi na kujeruhiwa begani alipokuwa njiani kuelekea kazini katika mtaa wa Karen jijini Nairobi. Akizungumza kwenye mahaojiano na vituo vya redio vinavyopeperusha matamgazo kwa lugha za eneo la […]

KENYA POWER YATANGAZA GIZA

Kampuni ya kusambaza umeme Kenya Power imeonya kuhusu ukosefu wa nguvu za umeme katika maeneo kadhaa nchini hii leo kutokana na ukarabati wa mitambo kuanzia saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.  Baadhi ya maeneo ambayo yataathirika na kukatizwa kwa umeme ni Pamoja na Nairobi, Bomet, Nandi, Kakamega, Homa Bay, Embu, Kirinyaga, na […]

IKULU NA AFISI YA NAIBU RAIS KUATHIRIKA ZAIDI KUFUATIA KUITHINISHWA KWA MSWADA WA ZIADA

Ikulu na afisi ya Naibu wa Rais zimesalia kuwa afisi zilizoathiriwa zaidi kufuatia kuidhinishwa kwa Mswada wa Uidhinishaji wa Ziada yaani suplementary budget (Na.2) wa 2024. Mswada uliopitishwa wiki jana unalenga kurekebisha mgao wa bajeti kwa mihimili mitatu ya serikali ili kushughulikia upungufu wa mapato wa Shilingi bilioni 344 kufuatia kukataliwa kwa Mswada wa Fedha […]

SITARUHUSU WATU KUCHAFUA JINA LA UHURU TENA – GACHAGUA

Naibu Rais Rigathi Gachagua ameapa kumtetea aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta dhidi ya yoyote ambayo yatadhalilisha urithi na utu wake. Akizungumza na vituo vya redio na runinga vya Mlima Kenya, jana jumapili Gachagua alisema umefika wakati nchi iache kumlaumu Uhuru kwa kila kinachotokea kwenda mrama. Gachagua ameongeza kuwa wakenya wanapaswa kumpa Rais mstaafu na familia yake […]

MJI ELDORET KUPANDISHWA HADHI AGOSTI 15

Ukabidhi wa hadhi ya jiji kwa mji wa Eldoret umeahirishwa kwa wiki moja hadi Agosti 15. Gavana wa Uasin Gishu Jonathan Bii leo Jumatatu amesema hafla hiyo iliyokuwa ifanyike siku ya Alhamisi, Agosti 8 imeahirishwa baada ya kushauriana na serikali ya kitaifa. Bii ameongeza kusema kuwa maandalizi yote ikiwa ni pamoja na kuutangaza mji huo […]

KUMBANDUA GACHAGUA KUTAUNDA SHUJAA KUTOKA KWA ‘MBABE WA KABILA’ – SENETA KAJWANG’

Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang’ amesema kuwa kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua mamlakani ni hatua mbaya ya kisiasa ambayo inafaa kuepukwa.Kwa maoni yake, kumtimua Gachagua afisini kutakuwa na athari mbaya kwa hali ya kisiasa inayompa umaarufu usio na msingi. Akihojiwa katika kituo kimoja cha runinga humu nchini Kajwang’ amebainisha kuwa kauli za Gachagua za […]

HIGHWAY YAPITA NA KITALE

Mabingwa wa Nairobi Highway walizamisha St. Joseph’s Kitale 1-0 na kuanza harakati zao za kuwania taji la taifa la kandanda kwa njia ya kutatanisha, Michezo ya Shule ya Sekondari ya Kidato cha Pili ilipong’oa nanga mjini Kisii Jumapili. Katika Uwanja wa Gusii uliojaa, timu hiyo inayonolewa na Beldine Odemba ilionyesha utulivu dhidi ya mabingwa hao […]

TUTAJARIBU TENA

Matumaini ya Ferdinand Omanyala kuandikisha historia ya kuwa Mkenya wa kwanza kabisa kutinga fainali ya Olimpiki ya mita 100 yalizimwa huku mwanamume mwenye kasi zaidi barani Afrika akiingia katika nafasi ya nane katika nusu fainali katika uwanja wa Stade de France mjini Paris. Omanyala, ambaye aliwasili Paris kama mwanamume wa pili kwa kasi zaidi duniani […]

CITY STARS WAPATA SARE MPYA

Kayole City Stars FC imeongezewa sare mpya na Katibu Mkuu wa Utawala wa Kitaifa Raymond Omollo, iliyowasilishwa Jumapili kwenye uwanja wao wa mazoezi huko Komarock, Nairobi. Ufadhili huo ni sehemu ya mpango unaolenga kukuza vipaji vya vijana, kutoa manufaa ya kiuchumi na kuzuia uvivu miongoni mwa vijana. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mratibu wa Mpango […]

SHABANA WAKO TAYARI KWA LIGI

Kocha Mkuu wa Shabana FC, Sammy ‘Pamzo’ Omollo anatarajia kwamba kikosi chake kitakuwa katika hali nzuri zaidi mwanzoni mwa msimu wa 2024/25, huku akipania kuanza kwa nguvu akiwa na nia ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu. Pamzo amekuwa na kazi ya kuunganisha pamoja timu iliyobadilishwa kwa kiasi kikubwa katika maandalizi ya msimu unaoendelea, na anafuraha […]