KENYA YAJIUNGA NA MATAIFA MENGINE KUSHEREHEKEA SIKU YA KUNYONYESHA

Lydia Kimani msimazi wa lishe bora amewarai waajiri kuwapa kina mama waliojifungua likizo ili waweze kuwanyonyesha wanao huku Kenya ikijiunga na mataifa mengine kusherehekea wiki ya kimataifa ya Kunyonyesha. Kimani ameongeza kuwa likizo ya uzazi ni haki na muhimu katika afya ya mama na ukuaji wa mtoto. Imetayarishwa na Janice Marete

RIPOTI YA MAHOJIANO YA MAWAZIRI KUWASILISHWA KESHO

Kamati ya uteuzi ya bunge la kitaifa ikiongozwa na spika wa bunge la kitaifa Moses Masika Wetangula inatarajiwa kuwasilisha ripoti ya mahojiano ya mawaziri hapo kesho, kabla ya vikao vya kujadili ripoti hiyo kufanyika siku ya jumatano wiki hii kuamua hatima ya mawaziri walioteuliwa na rais william Ruto. Spika wa bunge la kitaifa Moses Masika […]

GAVANA WANGA ANATOSHA

Viongozi wa kike wa chama cha ODM katika kaunti ya Homa Bay wamependekeza gavana Gladys Wanga kuchaguliwa kuwa naibu kiongozi wa chama hicho baada ya aliyekuwa naibu mwenyekiti wa chama hicho Ali Hassan Joho kuteuliwa kwenye baraza jipya la mawaziri la rais William Ruto. Wakiongozwa na kiongozi wa chama hicho wa kina mama tawi la […]

MBOGA ZAKATAA KUSHUKA

Wakenya wanaendelea kugharamika pakubwa katika ununuzi wa mboga, licha ya kushuka kwa bidhaa nyingi za matumizi ya nyumbani kiujumla. Katika mwezi wa Julai, bei ya kabeji, nyanya na vitunguu ilipanda kwa kasi ila kukawa na kushuka kwa bei za bidhaa nyinginek ama vile mahindi na mchele hali iliyosababisha mfumuko wa bei kushuka hadi asilimia 4.3. […]

“WAANZILISHI’ WA UDA WATOA KAULI KUHUSU MALALA

Saa chache baada ya chama cha UDA kumtimua Cleophas Malala kutoka kwa wadhifa wa kaimu katibu mkuu, baadhi ya wanachama wametangaza kukubali uamuzi huo na kupongeza uteuzi wa Hassan Omar. Kupitia taarifa, wanachama hao wakiongozwa na Joe Khalende wamesema zoezi hilo limefanywa bila miegemeo, wakitaka ukaguzi wa ununuzi wa vifaa vya chama wakati wa uongozi […]

WIZARA YA USALAMA YAOMBA FEDHA

Katibu katika wizara ya usalama wa kitaifa Raymond Omollo amesema kwamba serikali inahitaji kima cha shilingi bilioni 108 kutekeleza mageuzi katika idara ya polisi, ile ya magereza na idara ya huduma za vijana NYS ilivyopendekezwa na na jopokazi lililobuniwa na Raus William Ruto. Kwa mujibu wa Omollo, mageuzi hayo yatatekelezwa kwa kipindi cha miaka 4 […]

KVA YAISUTA SERIKALI YA NAKURU

Chama cha madaktari wa mifugo nchini KVA kimekosoa mipango ya serikali ya kaunti ya Nakuru kufunga kichinjio cha mamilioni ya fedha cha Naivasha ili kupisha ujenzi wa makazi ya bei nafuu na uwanja wa michezo. Kupitia taarifa, mwenyekiti wa chama hicho Kelvin Osore ameitaja hatua hiyo kuwa dharau kwa juhudi za serikali kuimarisha viwanda nchini, […]

FISADI HAWANA BAHATI, WAZIRI AONYA

Waziri mteule katika wizara ya kilimo Andrew Karanja ameonya kuwakabili watu fisadi kwenye wizara hiyo iwapo ataidhinishwa kuhudumu kama Waziri ili kuimarisha sekta hiyo ambayo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa Kenya. Akijibu swali lililoibuliwa na mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed kuhusu jinsi akavyowakabili matapeli kwenye sekta ya kahawa, miwa na hata majani […]

DUALE AKANA KUWAATISHIA WANAJESHI

Waziri mteule wa mazingira Aden Duale amepinga madai kwamba maafisa wakuu wa jeshi la ulinzi KDF walikuwa wakimwogopa alipokuwa Waziri wa ulinzi, na badala yake amesema kwamba huenda waliogopa mtindo wake wa uongozi. Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya uteuzi kubaini uwezo wake kwenye wizara mpya, Duale amesema mtindo wake wa uongozi umekuwa ule ule […]

AMPIGA MAWE ASKARI NANDI

Afisa wa polisi anauguza jeraha kichwani baada ya kupigwa mawe na mwanamume aliyekuwa akimzuia kufukua maiti katika kijiji kimoja eneo la Kaimosi, Kaunti ya Nandi. Maafisa wawili wa polisi walikuwa wamekimbia hadi kijiji cha Kiborgok ili kumzuia mwanamume asifukue mwili wa Darling Rukabite wakati kisa hicho kilipotokea. Timu hiyo ilifika eneo la tukio na kumkuta […]