WAZAZI NJIA PANDA MGOMO UKINUKIA

Wazazi walio na watoto katika shule za msingi na upili wanakabiliwa na njia panda kuhusu iwapo wawaruhusu wanao waelekee shuleni Jumatatu kwa muhula wa tatu au la, huku miungano ya kutetea maslahi ya walimu ikishikilia kuwepo kwa mgomo. Licha ya tume ya kuwaajiri walimu TSC kukubali kutekeleza awamu ya pili ya mkataba wa maelewano, walimu […]

VIONGOZI WATUMAI ODINGA ATASHINDA

Viongozi wakuu serikalini wamesema wana matumaini kwamba kiongozi wa Azimio Raila Odinga atafanikisha utatuzi wa changamoto nyingi zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi katika bara la Afrika, iwapo atachaguliwa kuwa mwenyekiti wa tum e ya umoja wa Afrika AUC. Wakiongozwa na Waziri wa mazingira Aden Duale, John Mbadi wa fedha na Alice Wahome wa ardhi, […]

WANAHARAKATI WATAKA UTEUZI WA JOHO UBATILISHWE

Kundi moja la wanaharakati limeelekea mahakamani kupinga uteuzi wa Ali Hassan Joho kuwa Waziri wa madini na raslimali za majini, likisema kamati ya uteuzi katika bunge la kitaifa lilipuuza notisi kadhaa zenye ushahidi kwamba Joho hakufaa kuteuliwa. Kulingana na kundi hilo, Joho hakufaa kuidhinishwa kwa misingi kwamba stakabadhi hitajika za masomo, na sasa wanaitaka mahakama […]

MAANDAMANO YA MATATU YAFUNGA NGONG ROAD

Shughuli za usafiri zimetatizika kwa mapema leo baada ya wahudumu wa matatu kufunga maeneo kadhaa ya barabara ya Ngong jijini Nairobi ikiwemo Dagoretti Kona na makutano ya Ring Road walipokuwa wakiandamana kulalamikia visa vya kuhangaishwa na maafisa wa polisi. Kulingana na wahudumu hao, polisi wamekuwa wakiwaitisha hongo kabla ya kuwaruhusu kuendesha biashara zao, wakishinikiza hatua […]

MAUAJI YA KWARE: MAHAKAMA YAWAPA POLISI DHAMANA

Mahakama kuu ya Milimani imewapa dhamana ya shilingi 200,000 kila mmoja maafisa wa polisi wanaodaiwa kuwasaidia washukiwa 13 akiwemo mshukiwa wa mauaji ya Kware Collins Khalusia kutoroka kutoka kituo cha Gigiri. Akitoa uamuzi huo, jaji wa mahakama hiyo Martha Naanzushi amekatalia mbali ombi la polisi kuwazuilia maafisa hao kwa siku 14 ili kukamilisha uchungizi dhidi […]

BEI GHALI YA MAJI YASIYOKUWEPO NAIROBI

Wakazi kutoka mitaa mbali mbali ikiwemo Mathare jijini Nairobi wamelalamikia kupanda kwa bei ya maji, kwa sasa wakilazimika kulipia shilingi 40 kwa lita 20 za maji, kutoka shilingi 5 za hapo awali. Hii ni baada ya ukosefu wa maji kushuhudiwa katika mitaa hiyo, hatua ambayo imewalazimu kutembea kwa mwendo mrefu kusaka bidhaa hiyo muhimu. Hata […]

MTIHANI BADO UPO

Baraza la Kitaifa la Mitihani la Kenya linasema kuwa wachezaji wanane wa timu ya taifa ya wanawake ya U-17, Junior Starlets, watafanya mtihani wao wa KCSE wa 2024 kama ilivyoratibiwa. Timu hiyo inatarajiwa kucheza Kombe la Dunia la FIFA U17 kuanzia tarehe 18 Oktoba hadi 3 Novemba, huku mitihani ya KCSE ikitarajiwa kuanza tarehe 4 […]

TUNAREJEA KWA KISHINDO

Bayer Leverkusen wameapa kufanya mambo makubwa tena msimu huu baada ya kushinda makombe mawili msimu jana ikiwemo taji la Bundesliga. Leverkusen wataanza msimu dhidi ya Borussia Moenchengladbach kesho, huku meneja Xabi Alonso akisema kuwa timu yake ina uwezo wa kutetea mataji yake. Mshambulizi wa Leverkusen, Nathan Tella pia ameiunga mkono timu yake kwa msimu mwingine […]

KALULU AJIUNGA NA JUVENTUS

Beki wa Ufaransa Pierre Kalulu amejiunga na Juventus kwa mkopo wa msimu mzima kutoka AC Milan. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ameichezea Milan mara 112 tangu aliposajiliwa mwaka 2020 baada ya kuhitimu kupitia akademi Lyon nchini ufaransa. Juventus wana chaguo la kumnunua Kalulu kabisa mwisho wa mkopo wake. Juve walianza kwa ushindi azma […]

BADO NAPUMZIKA

Bingwa wa Olimpiki wa mbio za mita 800 Keely Hodgkinson amefichua kwamba yuko mapumzikoni kwa salio la msimu huu baada ya kupata jeraha. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 22 alikua mwanamke wa tatu wa Uingereza kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki katika mbio za mita 800 huko Paris mwaka huu akifuata nyayo za Anne […]