MWANGA WA MWANGAZA WAZIDI KUWA GIZA

Baadhi ya wakaazi katika kaunti ya Meru wamekusanyika nje ya afisi ya gavana wa kaunti hiyo Kawira Mwanza kwa lengo la kumtimua katika afisi yake. Wakaazi hao wanasema kuwa ni kinyume na sheria kwa gavana huyo kurejea afisini baada ya kungatuliwa mamlakani. Imetayarishwa na Janice Marete

NI SHULE AU NYUMBANI?

Wazazi na wanafunzi humu nchini wamesalia katika njia panda kufuatia tangazo la KNUT kwamba wamesitisha mgomo wao huku muungano wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET wakianza mgomo wao rasmi hii leo katika kaunti mbali mbali humu nchini. Awali wizara ya elimu ilikuwa imewashauri wazazi kuwarejesha wanao shuleni kwa kutoa hakikisho la kuangazia […]

RUTO AAGIZA NYS KUWASAJILI WATU 20,000 MWAKA UJAO

Rais William Ruto ameagiza Huduma ya Vijana kwa taifa (NYS) kuongeza idadi ya walioajiriwa hadi 20,000 katika uhudumu wao ujao. Akizungumza alipoongoza gwaride la kufuzu kwa makurutu wa NYS huko Gilgil, Ruto amesema kundi la mwaka huu lilikuwa karibu watu 15,000 na anafurahia hilo. Alisema serikali itahakikisha vijana wengi zaidi wananufaika na mafunzo yanayotolewa na NYS. Imetayarishwa […]

MOTO WATEKETEZA MADUKA 10 HUKO HOMA BAY

Mali ya thamani isiyojulikana imeharibiwa katika kitongoji cha Rodi Kopany huko Homa Bay baada ya moto kuzuka katika kituo cha biasharaWalioshuhudia wamesema moto huo umesambaa kwa kasi na kuteketeza takriban maduka 10. Chifu wa eneo la Kanyango Samuel Nyagwara akithibitisha kisa hicho amesema kuwa chanzo cha moto huo hakijabainika ila uchunguzi umeanzishwa. Huku akithibitisha kuwa […]

WATU WENYE SILAHA WAUA MTU, NA KUIBA NG’OMBE 100 HUKO ISIOLO

Polisi wanasaka Kundi la watu wenye silaha ambao wamevamia kijiji cha Isiolo na kumuua mchungaji mmoja kabla ya kutoroka na ng’ombe 100. Kulingana na Polisi uvamizi huo umefanyika usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kambi Garba. Genge hilo limempiga risasi mchungaji mmoja kifuani walipovamia boma na kumuua papo hapo kabla ya kuondoka na ng’ombe […]

RUTO AONGOZA HAFLA YA KUFUZU KWA MAKURUTU WA NYS

Rais ruto anaongoza hafla ya 88 ya kufuzu kwa makurutu wa huduma ya taifa kwa vijana NYS inayofanyika katika chuo cha mafunzo ya kijeshi eneo la Gilgil kaunti ya Nakuru. Imetayarishwa na Janice Marete

NYANZA WARITHISHWA NA UTEUZI WA OWALO

Wakaazi wa eneo la Nyanza wameeleza kurithishwa na uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa habari na teknolojia Eliud Owalo kuhudumu kama naibu mkuu wa idara ya utekelezaji wa huduma katika afisi ya rais. Imetayarishwa na Janice Marete

MWANAMKE AMCHOMA KISU NA KUMUUA MUMEWE HUKO KASARAN NAIROBI

Mwanamke mmoja amekamatwa baada ya kudaiwa kumuua mumewe katika vita vinavyoshukiwa kuwa vya nyumbani huko Kasarani,kaunti ya Nairobi. Imebainika kuwa wanandoa hao walikuwa wamezozana na kupigana kabla ya mwanamume huyo kudungwa kisu kifuani. Kulingana na polisi, mwanamke huyo alitumia kisu cha jikoni kumchoma mwanamume huyo na kumuua papo hapo. Mwanamke huyo amekamatwa baadaye na kueleza […]

CHELSEA WATAZAMIA KUMSAJILI JADON SANCHO WA MAN-UNITED

Chelsea wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili Jadon Sancho kutoka Manchester United kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho wa majira ya kiangazi, Sancho alifungiwa nje ya kikosi cha United msimu uliopita baada ya kujibu mapigo kwenye mitandao ya kijamii kwa shutuma kutoka kwa meneja Erik ten Hag. Alijiunga tena na klabu ya zamani ya Borussia […]

GOR MAHIA WACHARAZA ELMEREIKH BENTU YA SUDAN KUSINI 5-1

Timu ya kenya Gor mahia imeicharaza Elmereikh Bentu ya Sudan Kusini mabao 5-1 katika mechi ya mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika ya CAF kwenye Uwanja wa Nyayo na kujipatia tiketi ya Kocha mkuu wa Gor Mahia Leonardo Neiva anasema wanapaswa kusalia wanyenyekevu na kuwa watulivu licha ya kuicharaza Elmereikh Bentu Baada ya […]