JIWE LA STONES YAIOKOLEA CITY ALAMA

Beki wa Uingereza John Stones aliikolea timu yake ya Man City katika dakika za lala salama na kuwapa sare ya mabao 2 dhidi ya Arsenal katika uga wa Etihad. Man city walichukua uongozi kunako dakika ya 9 kupitia msambuliaji wao matata Erling Halaand baada ya kumegewa pasi na kinda Savino, kabla ya Arsenal kusawazisha Ricardo […]

KARIOBANGI SHARKS WAREJEA KWA KISHINDO KPL

Ligi kuu ya soka nchini FKF premier ligi imeshuhudia mechi kadhaa mwishoni mwa juma, mechi za jana zikihusisha Shabana FC na Ulinzi Stars ambao walitoka sare ya mabao 2, katika uwanja wa Ulinzi sports complex. Hata hivyo, patashika ilishuhudiwa wakati wa mechi hiyo ambapo mashabiki waliharibu mali kadhaa uwanjani na kusababisha majeruhi kwa watu kadhaa. […]

FAMILIA YA NDUGU WA KITENGELA YAZUNGUMZA

Hatimaye familia ya ndugu wawili wa Kitengela waliokuwa wametoweka kwa mwezi mzima sasa imezungumza kwa mara ya kwanza tangu wawili hao wapatikane wiki jana. Kulingana na Abdirazak Longton ambaye ni nduguye Jamil na Aslam Longton, wawili hao walinyimwa chakula na kuteswa, mbali na kunyimwa haki nyingine za kikatiba walipokuwa wakezuiliwa na wanaoaminika kuwa polisi. Aidha, […]

DIDMUS- GACHAGUA ATAKUWA RAIA DISEMBA

Mbunge wa Kimilili kaunti ya Bungoma Didmus Barasa, amesema kwamba naibu rais Rigathi Gachagua atabanduliwa kutoka mamlakani kabla ya Disemba mwaka huu. Akihutubu katika eneo bunge lake, Barasa amesema hatua ya kumbandua Gachagua imechochewa na uamuzi wake wa kueneza siasa za kikabila mwaka jana na kulifananisha taifa na kampuni ya wenye hisa. Hata hivyo, wandani […]

MUSYOKA MAHAKAMANI KUPINGA MKATABA WA ADANI

Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka hii leo anatarajiwa kuwasilisha kesi mahakamani kupinga mkataba baina ya serikali na kampuni ya Adani ya India unaolenga kuipa kampuni hiyo usimamizi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA kwa miaka 30. Kwenye kesi hiyo, Kalonzo vile vile analenga kupinga mipango ya kuipa kampuni hiyo kandarasi ya […]

WABUNGE KUPINGA KUPOKONYWA DONGE LA NG-CDF

Wabunge wameapa kuwasilisha kesi katika mahakama ya rufaa kupinga uamuzi wa makamama kuu ulioharamisha sheria ya hazina ya kustawisha maeneo bunge NG-CDF, wakishikilia kwamba hazina hiyo imewanufaisha wakazi wa maeneo ya mashinani. Wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa ambaye pia ni mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro, wabunge wameitaka idara ya […]

WATATU WALIOTOWEKA WAKATI WA MAANDAMANO WAPATIKANA KAJIADO

Watu watatu waliotoweka wakati wa maandamano ya Kitengela kaunti ya Kajiado ambao ni ndugu wawili na mwanaharakati mmoja, wamepatikana wakiwa hai Watatu hao walitoweka tarehe kumi na tisa mwezi wa Agosti mwaka huu, wakati wa maandamano ya Gen Z ya kuishinikiza serikali iliyoko mamlakani kufanya mageuzi na kupunguza gharama ya Maisha. Gen Z walijitokeza pia […]

MAHAKAMA KUTOA UAMUZI KUHUSU INSPEKTA MKUU WA POLISI GILBERT MASENGELI

Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi wa iwapo itakumbatia uamuzi wake wa juma iliyopita wa kumhukumu naibu inspekta mkuu wa polisi katika kitengo cha polisi wa utawala Gilbert Masengeli, hii ni baada ya Masengeli kukabiliwa na maswali mahakamani akitakiwa kueleza ni kwanini alikaidi agizo la mahakama la kumtaka afike mbele yake kuhusiana na kutekwa nyara kwa ndugu […]

GACHAGUA ASIMULIA TUMAINI JIPYA

Naibu rais Rigathi Gachagua amedokeza kuwa viongozi kutoka eneo la mlima Kenya wanaounga azma yake ya kuwaunganisha viongozi wote wa eneo hilo huenda wakafanya maamuzi tofauti kwenye uchaguzi ujao wa mwaka wa 2027. Akiwahutubia wafanyibiashara katika soko la Markiti jijini Nairobi mapema leo, Gachagua amesema mara hii wameweka mpangilio wa kuhakikisha wanahamasisha wakazi kupiga kura […]

SHULE YA MUMBUNI MACHAKOS YAFUNGWA

Shule ya upili ya wavulana ya Mumbuni kwenye kaunti ya Machakos imefungwa kwa mda usiojulikana baada ya mali ya thamani isiyojulikana kuteketea kwenye moto uliochoma sehemu ya bweni, lenye wanafunzi 220 wa kidato cha pili na kidato cha tatu usiku wa kuamkia leo. Kwa sasa hakuna majeruhi wameripotiwa pale shuleni na wazazi wapo katika lango […]