SERIKALI KUDHIBITI ZIARA ZA MAWAZIRI

Serikali imezindua mfumo wa kidijitali wa usimamizi wa safari za nje za maafisa wa serikali kaitka juhudi za kuhakikisha usafiri unaowahusisha mawaziri na maafisa wengine wakuu katika serikali unadhibitiwa na kupigwa darubini na afisi ya utumishi wa umma. Naibu rais Rigathi Gachagua akizungumza kwenye hafla hiyo amesema kuwa mfumo huo utadhibiti utumizi mbaya wa pesa […]

MATOKEO YA MGOMO SHULENI

Athari za mgomo wa walimu wa shule za upili ambao umeingia siku ya 8 sasa zimeanza kuonekana wazi wazi, baada ya baadhi ya shule kuwataka wanafunzi waondoke na kurejea nyumbani hadi suluhu litakapopatikana. Baadhi ya shule hizo ni ile ya wasichana na wavulana ya Kenyatta katika kaunti ya Nakuru, ambapo wazazi wamefika shuleni humo mapema […]

KUPPET YAENDELEA KULEMAZA MASOMO

Mamia ya walimu wa shule za upili wameandamana kwa siku 8 hii leo na kulemaza shughuli za masomo kote nchini wakiitaka tume ya kuwaajiri walimu TSC itekeleze mtakaba wa maelewano baina yake na walimu. Mjini Kisii, walimu hao wamejitokeza katikati yam ji kutoa malalamishi yao ikiwemo kuwaajiri walimu wa JSS, kuwapandisha vyeo walimu waliohitimu na […]

AULIWA KWA SHOKA AKIJARIBU KUTENGANISHA VITA BAINA YA WANANDOA

Mwanamume mwenye umri wa miaka 28 amekatwa kwa shoka hadi kufa alipojaribu kutenganisha wanandoa waliokuwa wanapigana katika kijiji cha Buyinje, Musoli, Kaunti ya Kakamega. Marehemu ametambulika kwa jina la Moses Akumali. Mashahidi wamesema alikuwa akielekea nyumbani aliposhuhudia wanandoa wakipigana ndipo Kchukua uamuzi wa kuingilia kati ili kusitisha mapigano. Haijabainika ni nini kilisababisha mabishano na mapigano […]

WAFANYAKAZI WA ANGA KATIKA JKIA WAANDAMANA

Wafanyakazi wa usafiri wa anga chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (KAA) wamefanya maandamano katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA). Wakiwa na mabango, wafanyakazi hao wamelaani ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ambao utaipa kampuni ya Adani Group Holdings yenye makao yake makuu nchini India […]

GAVANA WA BUSIA ALALAMIKIA UPUNGUFU WA USHURU UNAOKUSANYWA KUTOKA KWA HOSIPITALI ZA UMMA KAUNTI HIYO

Wakaazi wa kaunti ya Busia wamelazimika kutafuta huduma za matibabu katika kaunti zingine kufuatia huduma duni katika hosipitali za umma za kaunti hiyo. Gavana wa kaunti hiyo Paul Otuoma amelalamikia kupungua kwa ushuru unaokusanywa kutoka kwa hosipitali za umma za kaunti hiyo kufuataia huduma duni zinazochangiwa na migomo ya mara kwa mara ya wahudumu wa afya. Imetayarishwa […]

AKAMATWA BAADA YA KUMUUA MWANAWE, 24, KATIKA MAPIGANO HUKO NANDI

Mwanamume mwenye umri wa miaka 48 amekamatwa kuhusiana na kisa cha kumdunga kisu na kumuua mwanawe mwenye umri wa miaka 24 katika kijiji cha Mosobecho, Kaunti ya Nandi. Mwathiriwa amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Kapsabet alipokuwa anatibiwa baada ya kujeruhiwa. Kulingana na ripoti ya polisi, kijana huyo aliuawa kwa kuchomwa kisu kifuani wakati […]

SINA MIUJIZA YA KULETA USHINDI

Erik ten Hag alisema yeye hana miujiza ya kutengeneza suluhu za haraka kwa Manchester United baada ya kushindwa kwa mabao 3-0 nyumbani na Liverpool siku ya Jumapili. Mholanzi huyo tayari hana presha ya kucheza mechi tatu tu kabla ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya pia kufungwa 2-1 wikendi iliyopita huko Brighton. […]

CHELSEA WARAMBWA

Chelsea ilikabiliwa na hali ya kuchanganyikiwa baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Crystal Palace, huku Newcastle ikiilaza Tottenham 2-1 huku Manchester United na Liverpool wakijiandaa kwa mchuano wao wa Ligi Kuu Jumapili. Chelsea inayonolewa na Enzo Maresca imeshinda mara moja pekee katika michezo mitatu ya kwanza ya ligi ya utawala wa Muitaliano huyo […]

KENYA YABEBA MEDALI SABA

Kenya ilikamilisha Mashindano ya Riadha ya Dunia ya Vijana chini ya miaka 20 katika nafasi ya tano kwa jumla ya medali saba. Huku pazia la mchuano wa siku tano likishuka katika uwanja wa Estadio Atlético de la Videna Lima, Peru, Kenya ilishinda medali tatu za dhahabu, tatu za fedha na shaba ili kukamilisha michuano hiyo. […]