29 BADO HAWAJULIKANI WALIKO, POLISI

Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja ametoa hakikisho kuwa polisi wanaendeleza uchunguzi ili kubaini waliko wakenya 29 waliotoweka tangu mwezi Juni, katika matukio ambako imeripotiwa kwamba wakenya Zaidi ya 40 waliuawa huku 22 wakitekwa nyara na kupatikana wakiwa hai. Akiwa mbele ya kamati ya usalama katika bunge la kitaifa, Kanja amekiri kuwa hajapata ripoti kamili […]

UGATUZI: SENETI, BUNGE ZAKOSA MWAFAKA

Huenda utoaji huduma katika serikali za kaunti ukaendelea kutatizika kutokana na ukosefu wa mwafaka miongoni mwa kamati ya upatanishi katika bunge la seneti na lile la kitaifa kuhusu kiwango cha mgao unaofaa kutumwa kwa serikali hizo. Mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa Ndindi Nyoro ameshikilia kuwa kuna upungufu wa shilingi bilioni 788 […]

HUENDA WENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE LA KITAIFA WASIOHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE WAKAKUFURUSHWA

Kiongozi wa wengi katika Bunge la Taifa Kimani Ichungwa ametoa onyo kali dhidi ya wananosusia vikao vya bunge. Wenyekiti wa kamati za bunge na manaibu wao walio na mazoea ya kutohudhuria vikao vya bunge wanakabiliwa na hatari ya kubanduliwa kwenye nyadhifa hizo. Matamshi hayo yanajiri baada ya kukosekana kwa wabunge ambao maswali yao yaliratibiwa kujibiwa […]

MAHAKAMA YAMRUHUSU GACHAGUA KUONDOA BAADHI YA KESI ALIZOWASILISHA MAHAKAMANI

Ni afueni kwa aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua baada ya mahakama kumruhusu kuziondoa baadhi ya kesi alizokuwa amewakilisha mahakamani. Gachagua kupitia kwa wakili mkuu wake Paul Mwite amewaambia majaji kwamba maswala mengine kama vile kuzuia kuapishwa kwa Kindiki kama naibu war ais yamepitwa na wakati. Imetayarishwa na Janice Marete

WAZAZI WATAKIWA KUWAJIBIKIA MAISHA YA WANAO

Wazazi wametakiwa kuwa waangalifu na kuwajibikia malezi ya wanao wakati huu wa likizo ndefu. Naibu kamishina wa webuye katika kaunti ya Bungoma Dickson Osundwa amewataka wazazi kuwaepusha wanao kuhudhuria hafla za disko matanga ambazo kulingana naye zimechangia ongezeko la uja ujito wa mapema kwqa wasichana. Osundwa aidha amesikitikia ongezeko la dhuluma za kijinsia eneo hilo […]

WIZARA YA AFYA YATAKIWA KULAINISHA MFUMO WA AFYA YA JAMII

Wito umetolewa kwa serikali kulainisha huduma za afya zinazotolewa chini ya bima mpya ya afya ya jamii SHA ili kuondolea mkenya mzigo wa gharama ya matibabu. Imebainika kuwa ipo hjaja ya serikali kuendelea kutumia mifumo ya afya iliyopo inapoendelea kulainisha mifumo ya sasa ili kuhakikisha wakenya wote wanaendelea kunufaika na huduma za afya kabla watatue […]

WIZARA YA AFYA KAUNTI YA TRANSNZOIA YAWAHAMASISHA WAKAAZI KUHUSU UMUHIMU WA CHANJO YA POLIO

Wizara ya afya katika kaunti ya Transnzoia inaendelea kuwahamasisha washikadau mbali mbali na wathiriwa wa kupooza kabla ya awamu ya pili ya chanjo dhili ya marathi ya pollio kuanza tarehe 9-13 mwezi huu kufanyika katika kaunti 9 kote nchini. Mshirikishi wa uhamasishaji katika maswala ya afya ya kaunti hiyo Leah Okumu amesema kuwa ni muhimu […]

AMORIM ANA KIBARUA KIGUMU

Ruben Amorim ndiye kocha wa hivi punde kuingia kwenye kiti moto cha Old Trafford kujaribu kurejesha nyota ya zamani ya Manchester United. Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ureno ataanza kuinoa klabu hiyo kuanzia Novemba 11 baada ya kumaliza muda wake wa mafanikio katika klabu ya Sporting Lisbon. Amorim anakuwa kocha wa sita wa […]

REAL MADRID WAZIDI KUZAMA

Miezi sita tu baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa, Real Madrid wanazidi kuzama katika hali mbaya. Wakifungwa 4-0 na wapinzani wao Barcelona kwenye Clasico mwishoni mwa Oktoba, Los Blancos wamelala kwa mara ya pili mfululizo wakiwa nyumbani Jumanne barani Ulaya, huku AC Milan wakishinda 3-1 kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu. Kikosi cha Carlo […]

WAZIRI WA MICHEZO AAHIDI KUONGEZA MGAO WA BAJETI KWA WANARIADHA

Katika hatua ya kuimarisha hadhi ya Kenya katika riadha duniani, Mawaziri wa Michezo Kipchumba Murkomen ametangaza mipango ya kuongeza mara tatu mgao wa bajeti kwa kambi za Riadha za Kenya (AK), kwa kulenga kukuza vipaji vya taaluma mbalimbali kwa mashindano makubwa ya kimataifa. Akizungumza katika ziara yake katika makao makuu ya Riadha nchini Kenya katika […]