NZOIA SUGAR WAZIDI KUTATIZIKA

Kikosi cha Ligi Kuu ya Taifa (NSL) kinachotatizika, Nzoia Sugar FC, kinakabiliwa na msukosuko uliosalia wa msimu huu, kufuatia kuondoka kwa wachezaji watano muhimu wa kikosi cha kwanza huku kukiwa na matatizo ya kifedha. Kocha mkuu wa timu hiyo, Charles Odero, alithibitisha kuachwa kwa wachezaji watano muhimu katika klabu hiyo, jambo lililoleta pigo kubwa kwa […]

NAIROBI CITY THUNDER WANGURUMA

Nairobi City Thunder iliendeleza msururu wa ushindi katika Ligi Kuu ya Kikapu ya Kitaifa ya Wanaume ya Kenya (KNBL) kwa matokeo ya kuvutia wikendi dhidi ya timu za varsity. Mabingwa hao watetezi walilaza USIU Tigers 85-67 Jumamosi kabla ya kusambaratisha Terror 96-48 ya Chuo Kikuu cha Nairobi siku ya Jumapili katika Ukumbi wa Gymnasium wa […]

BANDARI YAZINDUA WACHEZAJI WANNE WAPYA

Bandari FC, ilizindua wachezaji wanne waliosajiliwa wenye thamani ya jumla ya Ksh.2 milioni, huku wakiendelea na harakati zao za kuwania taji la ligi kwa mara ya kwanza. Klabu hiyo iliwakaribisha mshambuliaji matata John Mark Makwata kutoka Coastal Union ya Tanzania, Ali Halafu kutoka timu ya Daraja la Kwanza, Congo Boyz, Dennis Ng’ang’a aliyekuwa Gor Mahia […]

SERIKALI YAAHIDI KUBORESHA AFYA

Huku wengi wa wakenya wakilalamikia changamoto katika bima ya afya ya Taifa Care, serikali imeanzisha mikakati ya kutatua changamoto hizo mbali na kuboresha sekta ya afya kwa ujumla. Kwa mujibu wa naibu rais Kithure Kindiki, miongoni mwa changamoto zinazotishia ufanisi wa bima hiyo ni hatua ya wengi wa waliojisajili kukosa kulipa ada zao. Ameyasema haya […]

AHUKUMIWA MIAKA 150 KWA KUWAUA WANAWE

Mahakama ya Bomet imempa kifungo cha miaka 150 gerezani mwanamme mmoja baada ya kumpata na hatia ya kuwaua wanawe 3 mnamo mwaka wa 2019 katika kijiji cha Lelaitich kaunti ya Bomet. Akitoa hukumu hiyo, jaji Julius Ng’arng’ar ameyataja mauaji hayo kuwa ya kinyama na kusema kuwa hukumu hiyo itatumika kama funzo kwa walio na nia […]

MGOMO WA MADAKTARI WANUKIA KERICHO

Huenda shughuli za matibabu katika kaunti ya Kericho zikatatizika ndani ya wiki mbili zijazo iwapo serikali ya kaunti hiyo haitaingilia kati na kusitisha mgomo wa madaktari ambao wametoa notisi ya siku 14. Kupitia taarifa, viongozi wa muungano wa KMPDU wameilaumu serikali ya kaunti hiyo kwa madai ya kukosa kutekeleza mpango wa huduma uliokubaliwa, mfumo wa […]

HASARA YA MAMILIONI KUFUATIA MOTO KIAMBU

Polisi mjini Kiambu wanaendeleza uchunguzi katika mkasa wa moto ulioteketeza Zaidi ya nyumba 50 mjini humo na kuwaacha mamia ya wafanyabiashara wakikadiria hasara ya mamilioni ya pesa usiku wa kuamkia leo. Wengi wa waathiriwa ni wamiliki wa eneo hilo na wachuuzi ambao huweka bidhaa zao katika nyumba hizo, ingawa hakuna majeraha yaliyoripotiwa. Imetayarishwa na Antony […]

WAKAZI WA, SUNA MASHARIKI, WALALAMIKIA ONGEZEKO LA UHALIFU

Wakazi wa Kakrao, Suna Mashariki, kaunti ya Migori, wamelalamikia kuongezeka kwa visa vya uhalifu, huku Kaimu Chifu Wyckliff Onyango akisema zaidi ya watu 30 wameshambuliwa na kundi la vijana wasiojulikana. Wikiendi iliyopita pekee, watu kumi walilengwa, lakini washambuliaji hawaibi, hivyo nia yao haijulikani. Onyango ametoa wito wa ushirikiano kati ya wakazi na vyombo vya usalama […]

WAKAZI WA LITEIN WALALAMIKIA UHALIFU NA UKOSEFU WA MIUNDOMBINU

Baadhi ya wakazi wa Litein, Kaunti ya Kericho, wameitaka serikali ya kaunti kuingilia kati na kushughulikia ongezeko la visa vya uhalifu na hali duni ya miundombinu. Kulingana na wakazi eneo hilo halina taa za barabarani, jambo linalowafanya wafanyabiashara kuwa shabaha rahisi kwa wahalifu. Pia wamelalamikia ukosefu wa maji wa mara kwa mara, hali inayovuruga shughuli […]

WAATHIRIWA WA JANGA LA BWAWA LA MAI MAHIU WAKABILIWA NA CHANGAMOTO MPYA

Waathiriwa wa maafa ya bwawa la Mai Mahiu, yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 60, wamepata pigo jipya baada ya serikali kuzuia mashirika mawili ya hisani kujenga nyumba 14 kwa familia zilizoathirika. Serikali na wamiliki wa ardhi wanadaiwa kutofautiana kuhusu gharama ya ardhi, jambo lililokwamisha mpango wa makazi ya KSh. milioni 250. Mashirika hayo yameagizwa […]