UOKOAJI WAENDELEA KWENYE MGODI KAKAMEGA

Familia za waathiriwa waliokwama kwenye vifusi baada ya kuangukiwa na ukuta wa mgodi wa dhahabu katika eneo la Shinyalu kaunti ya Kakamega zimehakikishiwa kuwa shughuli za uokoaji zitaendelea hadi wapendwa wao watakapookolewa. Zoezi la uokoaji linaongozwa na maafisa wa usalama kwenye kaunti hiyo, wachimbaji migodi 12 wakihofiwa kukwama ndani ya mgodi huo. Jumla ya wachimba […]

SIWEZI TENA, GACHAGUA KUHUSU KUREJEA SERIKALINI

Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua amepuzilia mbali uwezekano wake kurejeshwa katika serikali ya rais William Ruto, anayosema ilimdhalilisha machoni pa wakenya. Akizungumza kwenye mahojiano na vituo vya redio vinavyopeperusha matangazo kwa lugha ya Kiluhya, Gachaga amekariri kwamba hawezi tena kufanya kazi na serikali hiyo anayoitaja kuwa fisadi. Wakati uo huo, Gachagua ameibua madai mapya kwamba […]

MWAMKO MPYA CHUONI MOI

Shughuli za masomo zinatarajiwa kuimarika katika chuo kikuu cha Moi na kutamatisha vuta nikuvute ambayo imekuwepo kwa miezi kadhaa, baada ya usimamizi mpya wa chuo hicho kuanza rasmi majukumu yake na kuahidi kuboresha huduma. Baada ya mkutano na wafanyakazi wa chuo hicho, mwenyekiti Profesa Noah Midamba na naibu chansela Profesa Kiplagat Kotut wameahidi mageuzi ya […]

POLISI MGONJWA ‘AWASHAMBULIA’ WAGONJWA BONDO

Maafisa wa idara ya upelelezi DCI katika eneo la Bondo kaunti ya Siaya wanachunguza kisa ambapo wagonjwa wawili wlaiokuwa wamelazwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Bondo wameshambuliwa na kudungwa kisu na afisa wa polisi ambaye pia alikuwa amelazwa hospitalini humo usiku wa kuamkia leo. Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi kaunti ya Siaya Serah […]

MBADI ABASHIRI UKUAJI WA UCHUMI

Taifa la Kenya litapata afueni ya kiuchumi kati yam waka 2034-48 wakati ambapo taifa halitakuwa na mikopo ya kulipia ya Eurobond. Haya ni kwa mujibu wa waziri wa fedha John Mbadi akizungumza kwenye kikao na wananchi katika bustani ya Jivanjee jijini Nairobi kuhusiana na bajeti ya kitaifa. Ameongeza kuwa taifa litaanza kulipia mikopo hiyo kuanzia […]

WANAFUNZI WAVAMIA HELB KUDAI MIKOPO

Athari za kucheleweshwa kwa mikopo ya bodi ya kufadhili elimu ya juu HELB zimeanza kujitokeza, baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi wakivamia afisi za bodi hiyo kushinikiza mikopo hiyo kutumwa. Wanafunzi hao ambao wamekita kambi nje ya jumba la Anniversary Towers kwa muda, wamelalamikia kushindwa kufadhili masomo yao kutokana na ukosefu wa fedha. […]

JUHUDI ZA KUBORESHA AFYA

Kama njia moja ya kulainisha utoaji huduma za afya kwa wakenya, kamati ya afya katika bunge la kitaifa imependekeza kubuniwa kwa tume ya huduma za afya itakayosimamia sekta hiyo. Mapendekezo hayo yamejiri wakati wa kikao cha kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wake mbunge wa Endebess Robert Pukose na jopokazi la watu 20 linaloendelea kupokea maoni […]

AFUENI KWA JAJI KULLOW

Jaji wa mahakama ya ardhi na mazingira aliyesimamishwa kazi Mohammed Kullow amepata afueni baada ya jopokazi lililobuniwa na Rais William Ruto kumwondolea tuhuma za utovu wa nidhamu, kushindwa na kazi na ukiukaji wa sheria za idara ya huduma za mahakama zilizokuwa zikimwandama. Baada ya uchunguzi kwa takribani mwaka mmoja, jopokazi hilo likiongozwa na jaji Patrick […]

KOECH: WAZIRI MUTURI ATAONDOLEWA MAMLAKANI

Kuna njama ya kumbandua mamlakani Waziri wa utumishi wa Umma, Justin Muturi, wakati wowote kuanzia leo, hay ani kwa mujibu wa Mbunge wa Belgut, Nelson Koech. Koech aidha ameibua madai kwamba Muturi amejiletea hili mwenyewe kutokana na ukosoaji wake wa hivi karibuni dhidi ya serikali kuhusu kesi za kutekwa nyara kwa wakenya na mauaji ya […]

MACHIFU WATANO WATEKWA NYARA NA AL-SHABAAB MANDERA

Machifu watano wa serikali wametekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa al-Shabaab katika kaunti ya Mandera. Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Mashariki, John Otieno, amesema kuwa machifu hao walikuwa wakielekea Elwak walipotekwa kati ya Bamba Owla na Ires Suki. Kwa mujibu wa mkuu wa polisi wa eneo hilo, timu ya usalama ya pamoja imepelekwa […]