VITAMBULISHO: VIONGOZI WAPINGA AGIZO LA RUTO

Viongozi mbali mbali akiwemo gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, wameendelea kupinga agizo la rais William Ruto la kutaka vikwazo viondolewe katika mchakato wa kutoa vitambulisho vya kitaifa kwa watu wanaotoka maeneo ya mipakani hasa Kaskazini mashariki, wakisema uamuzi huo utahujumu usalama wa taifa. Viongozi wengine ambao wamepinga agizo hilo ni maseneta wakiongozwa na mwenzao […]

NIKO TAYARI KUINGIA AUC, ODINGA

Ikiwa ni chini ya wiki moja kabla ya uchaguzi wa uwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika AUC kuandaliwa, waziri mkuu wa zamani Raila Odinga ambaye pia ni moja kati ya wawaniaji 3 kwenye kinyang’anyiro hicho, amesema atakubali matokeo ya uchaguzi huo. Akizungumza katika kongamano la viongozi wanawake wa chama cha ODM jijini Nairobi, Odinga […]

JUHUDI ZA SADC, EAC KUREJESHA UTULIVU DRC

Huenda machafuko yaliyo mashariki mwa taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC yakakomeshwa na utulivu kurejea nchini humo, kufuatia pendekezo la mazungumzo baina ya serikali ya DRC na wapiganaji wa M23. Kwa mujibu wa Rais William Ruto ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuna haja ya hatua za dharura kuchukuliwa ili […]

AUC: WANAWAKE ODM WAMWOMBEA ODINGA

Huku uchaguzi wa mwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika AUC ukikaribia, viongozi wanawake katika chama cha ODM wameandaa hafla ya maombi kwa ajili ya mwaniaji wa wadhifa huo Raila Odinga ambaye pia anahudhuria hafla hiyo. Uchaguzi huo utaandaliwa baadaye mwezi huu katika makao makuu ya Muungano wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa Ethiopia, […]

USAID: WAFANYAKAZI KAJIADO KUPEWA AJIRA MPYA

Wafanyakazi waliokuwa wakihudumu chini ya ufadhili wa shirika la USAID kwenye kaunti ya Kajiado wamepata afueni baada ya serikali ya kaunti hiyo kuwahakikishia kuwa watahamishiwa katika idara nyingine baada ya ajira yao ya shirika hilo kukatizwa. Akizungumza katika eneo la Kajiado ya kati, gavana wa kaunti hiyo Joseph Ole Lenku amewahimiza magavana wenzake kuiga mfano […]

MWANAMME AMUUA MKEWE, AJIUA MWINGI

Polisi katika eneo la Mwingi East wanachunguza kisa ambapo mwanamme mmoja ameripotiwa kumwua mkewe kwa kumkataka kwa upanga kabla ya kujitoa uhai kwa kunywa sumu katika wadi ya Moi. Kwa mujibu wa wakazi, wanandoa hao wamekuwa na mzozo wa mara kwa mara, wakisema polisi wamewahi kuingilia ugomvi wa wawili hao. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MASOMO YASITISHWA NAKURU HIGH BAADA YA GHASIA ZA WANAFUNZI

Masomo katika Shule ya Upili ya Nakuru yamesitishwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi kuandamana usiku wa kuamkia leo na kuharibu mali ya shule kutokana na malalamiko kuhusu chakula. Ghasia zilianza saa 8 usiku na kudumu kwa takribani saa sita kabla ya polisi kuingilia kati. Wanafunzi waliharibu madarasa, mabweni, na jengo la utawala, huku wengine […]

LIVERPOOL YAONDOLEWA KWENYE FA CUP NA PLYMOUTH

Liverpool ilitolewa kwenye FA Cup kwa kichapo cha 1-0 dhidi ya Plymouth, timu inayoburuza mkia kwenye Championship. Ryan Hardie alifunga penalti pekee, huku kocha Arne Slot akilipa gharama ya kupumzisha nyota wake. Licha ya kuwa na Luis Diaz na Diogo Jota, Liverpool walishindwa kutamba. Plymouth walipambana kwa ujasiri, huku kipa Connor. Imetayarishwa na Janice Marete

BANDARI YOUTH FC MABINGWA WA COAST BINGWA FEST

Bandari Youth FC walitawazwa mabingwa wa Coast Bingwa Fest jana Jumapili baada ya kushinda Simba Apparel 1-0 katika Uwanja wa Mbaraki, Kaunti ya Mombasa. Bao pekee la ushindi lilifungwa na Yusuf Ali, anayejulikana kwa jina la utani “China,” na kuipa Bandari Youth taji hilo. Fainali ilianza kwa kasi, ambapo Suleiman Kahema wa Bandari Youth alipiga […]

WABUNGE WAPUUZA UAMUZI WA MAHAKAMA DHIDI YA KENYA KWANZA

Baadhi ya wabunge wamepuuza uamuzi wa mahakama uliovua Kenya Kwanza hadhi ya chama chenye wingi bungeni, wakisema hauna athari yoyote. Mbunge wa Ugenya, David Ochieng, anasema uamuzi huo hauna maana kwa kuwa mabadiliko ya kisiasa tayari yamefanyika na Bunge linafaa kushughulikia mvutano huo. Mwakilishi wa Wanawake wa Laikipia, Jane Kagiri, kwa upande wake amesema kuwa […]