JEZI MPYA YA SHABANA

Timu ya Shabana ya Ligi Kuu ya FKF-Kenya itazindua jezi za msimu huu zinazosubiriwa kwa hamuJumapili saa 9.00 asubuhi katika hafla ya kupambwa itakayotangulia mchuano wao wa Kombe la FKFdhidi ya Plantech FC inayoshiriki Ligi ya Daraja la Pili ya Naivasha. Tangazo hilo linafuatia mawasiliano ya awali ambapo Katibu Mkuu wa klabu Elizaphan Keramaalidokeza uwezekano […]

TUTAUNGA KOCHA MPYA MKONO

Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) Hussein Mohammed amethibitisha uungaji mkono waserikali kwa shirikisho hilo na michezo. Siku ya Jumatatu baada ya kuzindua uteuzi unaotarajiwa na unaokisiwa sana wa Benni McCarthy waAfrika Kusini, Mohammed alisisitiza dhamira ya serikali ya kuendeleza soka nchini Kenya. Tangu kuchukua wadhifa huo, utawala wa Mohammed umepokea maoni chanya […]

KOMBE LA RAGA LAFIKA MWISHO WEEKEND HII

Msimu wa kawaida wa Kombe la Kenya 2024/25 unafikia kilele chake wikendi hii, huku Pirates yaPwani Kusini wakikabiliwa na wakati mahususi katika msimu wao wa kwanza.Wakiwa wamejikita mkiani mwa jedwali wakiwa na pointi tisa pekee, pirates lazima watoe uchezajiwa karibu wa kustahimili nafasi yoyote ya kuendelea kuishi. Imekuwa mwanzo mgumu katika raga ya ligi kuu […]

UGONJWA TATA KISII WAANZA KUBAINIKA

Huenda suluhu likapatikana kwa ugonjwa usiojulikana ambao umezua hofu katika katika eneo la South Mugirango kaunti ya Kisii, bada ya uchunguzi kuuhusisha na maji machafu. Kupitia taarifa, katibu katika wizara ya afya Mary Muthoni amesema uchunguzi wa sampuli zilizokusanywa zimeonyesha uwepo wa kinyesi kwenye mojawapo ya visima vya maji eneo hilo. Huku akisema uchunguzi unaendelea, […]

RAIS RUTO AMWOMBOLEZA MALULU

Rais William Ruto amehusisha hatua zilizopigwa katika sekta ya elimu na aliyekuwa mbunge wa Malava Malulu Injendi, akisema walishirikiana ili kutatua changamoto zilizokuwa zikivikumba vyuo vikuu nchini. Rais ameyasema haya kwenye hafla ya mazishi ya mbunge huyo katika eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega, akimtaja kuwa shujaa wa imani. Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAKAZI WA NAMWELA WAPOKEA UFADHILI WA MBUZI

Ni afueni kwa wakazi wa wadi ya Namwela kaunti ya Bungoma, baada ya kupokezwa mbuzi wa maziwa kutoka kwa mwakilishi wa wadi hiyo Charles Nangulu, ambaye amesisitiza kuwa ufigaji na kilimo ndio njia mwafaka ya kuboresha uchumi wao. Akizungumza kwenye hafla hiyo, mwakilishi wadi huyo amewahimiza walionufaika kuwatuza mifugo hao kama njia mojawapo ya kuondoa […]

JUHUDI ZA KUREJESHA UTULIVU KISII-NAROK

Katika juhudi za kurejesha utulivu na kuimarisha mshikamano miongoni mwa jamii zinazosihi kwenye mpaka wa kaunti za Narok na Kisii, kamishna wa kaunti ya Narok Kipkoech Lotiatia amezitaka jamii hizo kusitisha uhasama na kukumbatia mazungumzo. Akizungumza afisini mwake, kamishna huyo amesema polisi wanaendesha uchunguzi ili kurejesha ng’ombe walioibwa Pamoja na taarifa za mashamba kuchomwa moto. […]

MLINZI WA USIKU AUAWA MACHAKOS

Hofu imetanda miongoni mwa wafanyabiashara mjini Machakos wanaohofia usalama wao, baada ya mlinzi mmoja wa usiku kuuawa na majambazi waliovamia duka la nguo usiku wa kuamkia leo. Imearifiwa kuwa majambazi wamevamia duka hilo na kupora nguo na bidhaa nyingine za thamani baada ya kumwua mlinzi huyo ambaye mwili wake umepatikana nje ya duka hilo. Wenyeji […]

MIGOMO YAENDELEA KULEMAZA MATIBABU

Huduma za matibabu katika kaunti ya Nairobi na maeneo mengine ya taifa zimeendelea kutatizika kufuatia mgomo wa mamia ya wahudumu wa afya walioajiriwa chini ya mpango wa afya kwa wote UHC, ambao wameandamana jijini Nairobi kushinikiza serikali iwape ajira ya kudumu. Wahudumu hao kutoka nje na ndani ya Nairobi, wametatiza shughuli za uchukuzi katika kituo […]

USIBAKI TU ODM, WAJACKOYA AMSHAURI ODINGA.

Huku kinara wa ODM Raila Odinga akiendeleza vikao vya mashauriano kabla ya kutoa mwelekeo wake wa kisiasa atakaochukua, kinara huyo sasa ametakiwa kutofanya mashauriano na wanachama wa ODM pekee na badala yake awashirikishe wakenya wote. Katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini, kiongozi wa chama cha Roots George Wajackoya, amemtaka Odinga kufanya mashauriano na […]